The House of Favourite Newspapers

Fella, Thabit Nusura Wazichape Msalani

Said Fella na wanamuziki wa Yamoto Band.

Na ISSA MNALLY| IJUMAA WIKIENDA|OVER ZE WEEKEND

WAMILIKI wa Makundi ya Taarab, Thabit Abdul wa Wakali Wao na Said Fella wa Yah TMK nusura wazichape msalani kisa kutaka kuchukuliana wanamuziki. Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika onyesho la pamoja la bendi hizo ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar.

Thabit Abdul.

Wawili hao walikutana msalani wakati Fella akitoka na Thabit akiingia ndipo songombingo lilipoanzia huku Thabit akimlalamika Fella kuzungumza na wanamuziki wake akiwalaghai kuwachukua.

Hata hivyo, songombingo hilo liliwahiwa na mashabiki kuingilia kati na kuwaachanisha. Baada ya kutulia kwa tafrani hiyo, Over Ze Weekend lilimsogelea Thabit na kumhoji kulikoni:

“Fella ameniudhi sana, alikuwa akizungumza na baadhi ya wanamuziki wangu kwa lengo la kuwashawishi wajiunge naye,,” alisema Thabit.

Fela.

Naye Mkubwa Fella alisema: “Siwezi kumfanyia unyambilisi wa kumwibia wanamuziki, najua alipotokea na namchukulia kama mwanangu tu wala asipaniki.

 

Comments are closed.