Nyoshi Alilia Kupiga Shoo Dar Live
Na ISSA MNALLY| GAZETI LA UWAZI| UWAZI SHOW BIZ
RAIS wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma‘, Nyoshi El Saadat ameibuka na kusema kuwa miongoni mwa vitu anavyotamani na kulilia kwa sasa ni kupiga shoo kwenye Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem ambapo hupata fursa ya kukutana na mamia ya mashabiki wa kazi zao tofauti na kwenye kumbi nyingine za starehe.
Akichonga na Uwazi Showbiz ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Nyoshi aliongeza kuwa kufanya shoo mbele ya watu wengi ni jambo Nyoshi alilia kupiga shoo Dar Live ambalo huwa analifurahia zaidi ndiyo maana anatamani siku za hivi karibuni afanye hivyo Dar ili wakutane na mashabiki wao wengi.
“Unajua kunamzuka wa tofauti kupiga shoo kwenye ukumbi kama Dar Live na kwenye kumbi nyingine ndogo, ukumbi mkubwa unafurahia watu wanaimba pamoja nasi lakini kwenye kumbi zingine unakuta watu wanatusikiliza tu tukiimba huku wao wanastarehe kwa vinywaji. Nimepamis sana Dar Live, nitahakikisha hivi karibuni nafanya onesho na vijana wangu pale,” alisema Nyoshi.
Comments are closed.