The House of Favourite Newspapers

Belle 9 Atinga Mwanza Kumfariji Jetman

Na MAYASA MARIWATA| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ hivi karibuni aliamua kufunga safari mpaka jijini Mwanza kwa ajili ya kumjulia hali Mwanamuziki Dolphin Pose ‘Jetman’ ambaye yupo kitandani kwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo uliomsababishia kupooza miguu.

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, dairekti kutoka kwenye jiji la miamba,  Belle 9 amesema kwa muda mrefu amekuwa akiguswa na maradhi yanayomsumbua mkali huyo wa Muziki wa Rege na Dancehall aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa ukiwemo wimbo uitwao Huyu Demu.

“Jetman kateseka sana kitandani jamani, miaka kama mitano sasa na anahitaji msaada kutoka kwetu hasa familia yake ya muziki namaanisha wanamuziki na wadau wake wote.

Nimeamua kuja kumtembelea ili angalau nimpe faraja kuwa ipo siku atapona na maradhi hayo yatageuka kuwa historia kwake,” alisema Belle 9 na kuongeza kuwa;

“Jetman anashindwa kupona kwa sababu hana pesa ya kumuwezesha kwenda kupata matibabu nchini India. Pesa inayotakiwa ni takriban shilingi milioni 12 hivi, kwa hiyo nawaomba wadau wajitoe ili tuweze kumsaidia ndugu yetu.”

 

Comments are closed.