The House of Favourite Newspapers

Kaka Sungura Afunguka Kutoka na Avril

Judith Nyambura ‘Avril’.

Na Mwandishi Wetu/GPL

MKALI wa michano kutoka Kenya, Kelvin Ombima ‘Kaka Sungura’ amefungukia juu ya tetesi za kutoka na mwanamuziki mrembo anayesumbua katika ardhi hiyo ya Uhuru Kenyatta, Judith Nyambura ‘Avril’ kuwa si za kweli bali ukaribu na mwanadada huyo ni wa kikazi tu.

Kelvin Ombima ‘Kaka Sungura’.

Akipiga stori moja kwa moja kutoka Kenya na Uwazi Showbiz, Kaka Sungura alipobanwa afungukie kujiachia kimalovee na Avril ambaye ni balozi pia wa Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya Itel, aliongeza kuwa mwanadada huyo ni miongoni mwa wasanii anaowasimamia chini ya lebo yake ya Kaka Empire kwa hiyo hata wanapokuwa karibu ni kwa sababu ya kazi tu na si vinginevyo.

“Mimi na Avril tupo karibu kwa sababu ya kazi mazee na si mapenzi, yule ni msanii wangu ninayemsimamia, kwa hiyo nasimama kama bosi wake lakini muziki hautufanyi kuwa mbali ndiyo maana watu wanahisi naruka naye, lakini si kweli,” alisema Kaka Sungura.

 

Comments are closed.