Wema Ahofia Usalama Wake

Wema Sepetu akiwa na Godbles Lema Mbunge wa Arusha mjini.

DAR ES SALAAM: Miss Tanzania 2016, ambaye pia ni muigizaji nyota, Wema Sepetu, amesema amepunguza matembezi na baadhi ya marafiki kwa sababu ya kuhofia usalama wake, hasa katika kipindi hiki cha mpito.

Wema Sepetu.

Uchunguzi uliofanywa na Risasi Mchanganyiko unaonyesha kuwa staa huyo mkubwa, ambaye wiki chache zilizopita alihama kutoka chama chake cha CCM na kujiunga na Chadema, haonekani kwenye matukio mengi ya kistaa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Wema akiwa na mama yake.

Katika uchunguzi huo, ilibainika kuwa muigizaji huyo haonekani kwenye matukio kama kumbukumbu ya kuzaliwa, send off na hata kwenye kumbi za starehe kama ilivyokuwa, huku baadhi ya watu wake wa karibu wakisema hata simu yake, haipatikani kirahisi. “Kuna kitu naona hakiko sawa kwa Wema, sisi wenyewe tunashangaa maana tunajua yule ni mtu wa kujichanganya na marafiki, lakini pia anapenda kula bata, sasa ghafla tu ametoweka, hapatikani, tukimpigia wakati mwingine hapokei, yaani anatuchanganya kabisa,” alisema mtu wake huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake. Risasi Mchanganyiko lilimpigia staa huyo ili kupata maoni yake, lakini simu yake haikupatikana, jambo lililolifanya gazeti hili kumtembelea nyumbani kwake wiki iliyopita huko Ununio, nje kidogo ya jiji, ambako lilimkuta dada wa kazi, aliyedai kuwa bosi wake alikuwa ametoka na angeweza kupatikana jioni. Katika kujaribu tena simu yake, alipatikana na alipoulizwa kuhusu kupotea kwake, alisema; “Ni kweli, nimejipoteza katika macho ya watu, nahofia usalama wangu kwa sababu hali si nzuri, siyo tu nimepotea, lakini pia nawadelete (kuwafuta) baadhi ya marafiki, siyo unakuwa na marafiki wengi ambao hauna faida nao.” “Hata katika kutoka, sitokitoki ovyo kama zamani, ni lazima nione kuwa mtoko huo una masilahi kwangu ndiyo natoka, siwezi kwenda sehemu ambayo haina faida na mimi katika wakati kama huu, kwa hiyo naomba uelewe kuwa hiyo ndiyo sababu ya mimi kutoonekana.” Wema Sepetu aliyekuwa miongoni mwa wasanii kutoka Bongo Muvi waliokipigia debe Chama Cha Mapinduzi (CCM), alikihama chama hicho muda mfupi baada ya kupandishwa mahakamani, akituhumiwa kutumia madawa ya kulevya, akiwa ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kabisa kutajwa kwenye sakata la madawa ya kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

ITAZAME VIDEO YA HAMORAPA KUTANGAZA KUMUOA WEMA.
Toa comment