Kipi Bora Adungwe Mimba, Atoroshwe au Umuozeshe?

Na HARMORAPA| GAZETI LA AMANI| SINDANO ZA MASTAA

MPENZI msomaji natumia fursa hii kukukaribisha kwenye safu hii bora kabisa ya Sindano za Mastaa. Wiki iliyopita ulikuwa na staa wa Bongo Muvi kwa upande wa vichekesho, Tausi Mdegela.

Wiki hii upo na staa wa Bongo Fleva, Athumani Omary ‘Harmorapa’ ambaye kila siku amekuwa akitengeneza vichwa vya habari kutokana na matukio yake.

NIANZE KWA KUSEMA…

Kabla ya kuingia kwenye mada yangu, naomba kuwasalimu mashabiki wangu, wakubwa kwa wadogo kisha tuingie kwenye mada yetu kama ifuatavyo; Jamii yetu kwa sasa imekuwa na tabia ya wazazi kuwakataa wachumba wa watoto wao, hata kama wamependana wao na wameamua kwenda kujitambulisha nyumbani ili wazazi wawape baraka za kufunga ndoa.

ANAWEZA KUMTOROSHA

Hivi tatizo la watoto liko wapi kama wameridhiana, wamependana na wameamua kupata baraka za wazazi? Ukiangalia si ajabu mwanaume ana uwezo wa kumshawishi au kumtorosha mwanamke lakini kwa kuwa ana mapenzi ya dhati na adungwe mimba, atoroshwe au umuozeshe? heshima juu ya mwanamke basi anaamua kuja kujitambulisha, leo unamkatalia, nini maana yako?

SABABU ZENYEWE ZA AJABU

Ukiangalia sababu za baadhi ya wazazi ambao wanakataa kuwaozesha watoto wao eti ni kwa sababu mwanaume hana hadhi, pesa, kazi nzuri, elimu ya kutosha na mambo mengine.

MALI SI KIGEZO BALI UTU Hivi kweli!

Hivyo vitu ndivyo vigezo sahihi vya mtoto wako kuolewa? Mbona mzazi unakosea na unasahau kigezo kikubwa kuliko vyote cha utu? Hivi itakuwaje kama mwanao ataolewa na mtu ambaye ana kila kitu lakini hana utu, upendo na hapendi ndugu.

UTOFAUTI WA MASKINI

Hata wewe mama au baba ambaye ulitegemea kuolewa kwa mwanao itakuwa ni neema kwako lakini kwa tabia ya mwanaume uliyemuoza mwanao, kuanzia mwanao na wewe mzazi umeula wa chuya, ni mara mia ungemuozesha kwa maskini ambaye anaweza kugawana na ndugu zake hata kama ana kiazi kimoja.

ATOROSHWE AU ADUNGWE MIMBA?

Nakuuliza wewe mama au baba ambaye unamkatalia mwanao kuolewa na mchumba ambaye amemchagua mwenyewe, kipi bora? Mwanao akutambulishe ampendaye, atoroshwe, adungwe mimba au aachwe? Kwa mzazi mwenye busara, muelewa na anayejua maisha yaliyo kwake ni heri mwanaye aolewe kwa baraka zake hata kama watakuwa wanashindia ugali wa chumvi kuliko kupigwa mimba, kutoroshwa au kutelekezwa na mwanaume ambaye hafahamiki kwake, kwanza ni aibu.

UTU HAUUZWI

Nadhani ni wakati sasa umefika wa wazazi kuwapa nafasi watoto wenu kuolewa na wanaume wanaowapenda, siyo kwa kuangalia pesa, elimu, mali au kazi nzuri kwani hivyo vyote vinatafutwa lakini kamwe utu hautafutwi wala hauuzwi sehemu yoyote. Ndiyo maana hata mimi nimetangaza kuwa niko tayari kumuoa Miss Tanzania mwaka 2016, Wema Sepetu. Kwa maoni na ushauri tembelea ukurasa wetu wa Gazeti la Amani kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Insta:mimi_ na_uhusiano au unaweza kujiunga na M&U WhatsApp kupitia 0679979785.
Toa comment