The House of Favourite Newspapers

Mama Kanumba, Mrithi wa Mwanaye Kimenuka!

Mama Kanumba (Flora Mtegoa) na Fredy Swai.

SIKU chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumtambulisha mrithi wa mwanaye kuwa ni Fredy Swai, wametibuana na sasa kila mmoja yuko kivyake chanzo kikidaiwa kuwa ni masuala ya fedha.

Chanzo kilicho karibu na wawili hao kilimwaga ubuyu kuwa, hali ya kutibuana ilikuja baada ya mama Kanumba kutumia jina la kijana huyo katika kutafutia pesa kwa madai kuwa wanataka kuandaa fi lamu na mchezo uliposhtukiwa, Fredy akamaindi na kununa.

Baada ya kupata ubuyu huo gazeti hili lilimtafuta mama Kanumba aliyekuwa na haya ya kusema:
“Nadhani mimi sina bahati, huwa nawapokea watu kwa moyo wote kisha wananiona sifai, huyu kijana huenda utoto unamsumbua.” Kwa upande wake Fredy alisema:
“Kuna mambo madogo tumekwazana lakini sipo tayari kuyaongelea kwa sasa, namheshimu mama Kanumba kama mzazi wangu.”

 

Comments are closed.