The House of Favourite Newspapers

Sababu 10 Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito

0

WAJAWAZITO wengi huugua wakati wakiwa na ujauzito. Zipo Sababu zinazofanya kutokea kwa maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba.

Kuna matatizo mengi ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu kwa mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito.

Tofauti kati ya watu hao wawili hupatikana baada ya uchunguzi. Maumivu ya tumbo kwa mjamzito ni changamoto kwa sababu wengi hupatwa na  kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi. Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma  viungo vingine kando ndani ya tumbo.

Upungufu wa damu na leukocytosis ni  kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa damu au maradhi.

Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ambayo huchukua muda wa siku mbili au tatu na kiasi kidogo cha damu ukeni hutoka. Mara nyingi kiasi hiki cha damu huwa ni kidogo na hutokea kati ya siku saba au 12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa, mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi.

Hivyo, wagonjwa  mara  nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida. Mimba iliyotunga nje ya mfuko Tatizo hili husababisha maumivu kwa akina mama wengi walio na mimba nje ya mfuko wa mimba. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni cha HCG.

Uzuri ni kwamba tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji. Kutoka kwa mimba Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya akina mama katika nchi zinazoendelea. Uvimbe kwenye mirija ya mayai (Ovarian cyst) Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha.

Hata hivyo, unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito. Kujizungusha kwa mirija ya mayai (Ovarian torsion) Hii hujitokeza mara chache. Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika miezi ya awali.

Kidole tumbo (Appendicitis) Kidole tumbo hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasuaji. Mara nyingi wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji. Mawe kwenye mfuko wa nyonga Lakini pia kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo.

Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya kupimwa na kipimo cha Ultrasound na matibabu yake hutegemea na dalili alizonazo mgonjwa. Uvimbe (Inflammation) kwenye mfuko wa nyongo Hili ni tatizo la ghafla linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati mwanamke ana mimba. Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo.

Matibabu yake hutumika dawa za kuua bakteria yaani Antibiotics. Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati wa mimba. Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na Round Ligament.

Ligament hii ndiyo inayoshikilia mfuko wa uzazi. Mfuko wa uzazi unavyozidi kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.

Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili. Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana  kwa mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia mionzi vitumike tu pale inapohitajika kwa mama mjamzito.

Leave A Reply