Q Chillah Kumwanika Mpenzi Wake
Na GABRIEL NG`OSHA| GAZETI LA AMANI| SHOWBIZ XTRA
MSANII wa Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ anayetamba na Wimbo wa Koku na Sungura, Aprili 30, mwaka huu amejipanga kumtambulisha rasmi mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Lizy kwenye ‘event’ maalumu ya Miaka 15 ya Harakati za Q-Chillah.
Akizungumza na Show Biz Xtra, Chillah alisema kuwa Lizy ni mwanamke ambaye amemvumilia sana katika magumu yake, hivyo hana budi kumtambulisha rasmi kwenye umma, ikiwezekana kwa kumvisha pete.
“Nimepita na Lizy kwenye magumu mengi sana, lakini hakuwahi kuniacha, amekuwa mshauri wangu na rafiki yangu, sasa ni muda muafaka wa kumtambulisha rasmi, aidha kwa kumvisha pete au kitu kingine