KIKOSI cha Yanga kimepata ahueni kidogo baada ya kipa namba moja wa MC Alger ya Algeria, Faouzi Chaouchi, kuhukumiwa kwenda jela miezi sita, hivyo hataweza kukaa langoni kesho Jumamosi katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa nchini Algeria.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, kipa huyo ndiye aliyekaa langoni kwa dakika zote na kuruhusu bao moja lililoipa ushindi Yanga.
Kukosekana kwa Chaouchi katika mchezo wa kesho, kunatoa nafasi kwa kipa namba mbili wa timu hiyo, Chalr Farid kukaa langoni.Kwa mujibu wa televisheni moja ya nchini Algeria, Februari 7, mwaka huu, Chaouchi alimpiga polisi wakati wa ukaguzi kabla ya kuingia uwanjani kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Hussein Dey uliopigwa kwenye Uwanja wa Julai 5. Mbali na kifungo hicho, pia amepigwa faini ya dola 45 (Zaidi ya 900,000)
Omary Mdose, Dar es Salaam, Championi Ijumaa