The House of Favourite Newspapers

Afa Kisa Goli la Simba

0

STORI:GLADNESS MALLYA | Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Kifo popote! Mechi ya Simba na Mbao FC iliyochezwa Aprili 10, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza imesababisha kifo cha Hamis Maige ‘Bika’ mkazi wa Ifakara, Morogoro ambaye ni shabiki wa Timu ya Simba baada ya kupata mshtuko kutokana na mabao ya ghafl a iliyoipata timu hiyo.

Kaka wa marehemu aitwaye Hashim Manondo alieleza kuwa siku ya mechi, Hamis alikuwa
akikuwa akifuatilia mchezo huo kwa ukaribu huku wakiwasiliana kwa simu kwani yey
alikuwa eneo jingine.
“Yeye alikuwa anatazama mpira kwenye kibanda cha kuoneshea mpira, Simba tulipofungwa gori mbili bila, akanipigia simu na kuniambia bro tunalala.

“Nikampa moyo, nikamwambia tutarudisha maana Simba ndiyo kawaida yake, mnaweza mkatangulia lakini baadaye inayapangua na kuongeza.

“Sasa baadaye tulipokomboa na kuongeza, aliruka sana juu na aliporudi chini ndiyo akapata stroke.,” alisema kaka huyo wa marehemu.

Baada ya kupata mshtuko huo alipelekwa katika Hospitali ya St. Francis iliyopo Ifakara ambako aliendelea kupatiwa matibabu lakini alifariki dunia Jumanne usiku na kuzikwa Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kwa Manyuka yaliyopo hapohapo Ifakara.

Kaka wa tumbo moja wa marehemu aitwaye Hussein Maige alithibitisha kifo cha mdogo wake kilichotokana na goli hilo na kusema marehemu ameacha watoto wawili.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlabani A, Hassan Mohamed alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema alisikitishwa na kifo hicho kwani badala ya furaha imekuwa ni huzuni.

“Ni kweli Hamis amefariki dunia baada ya kupata mshtuko kutokana na bao la tatu walilopata Simba ambayo ni timu aliyokuwa akiishabikia na papo hapo akapata strock, akapelekwa hospitali akapatiwa matibabu Jumanne mchana akawa anazungumza lakini akafariki usiku wake,” alisema Mwenyekiti Hassan.

Leave A Reply