The House of Favourite Newspapers

Mpenzi Wangu Anapenda Ngono tu!

0

Na Anko Nangale/GPL

HABARI anko? Nina mpenzi wangu nimeishi naye miaka miwili simuelewi, anapenda ngono tu. Nimeshachoka kuishi maisha ya kibachela, nimemuomba japo aende kwetu ajulikane anasema ningoje, nifanyeje anko na miaka inasonga?

Jibu: Kwa muda ulioishi naye, huna sababu ya kuwa na hofu kama umeambiwa usubiri labda kama hakuonesha dalili zozote njema tangu mnaanza hadi sasa. Kama hakuonesha na kila siku amekuwa akikuhitaji tu kwa ajili ya ngono na baada ya hapo haongelei maisha wala uhusiano wenu basi una kila sababu ya kujiweka mbali naye.

Yamkini alikuwa kama amekuwa akiendelea kuzungumzia maisha yenu na ukimtazama kweli ana maanisha basi huna budi kumsubiri na kumsaidia kimawazo na kila kitu ili muweze kufi kia malengo yenu. Usiwe na haraka kama unaona ana dhamira ya dhati  na wewe. Mpe muda, mtafi kia kilele cha mafanikio.

Leave A Reply