The House of Favourite Newspapers

Mapenzi ni Uwekezaji, Umewekeza na Nani?

0

KUISHI na mtu kama mpenzi wako, kunahitaji imani ya hali ya juu. Unapanda ‘mbegu ya uzima’ na mtu ambaye mmekutana pengine ukubwani. Hujui alikotoka, hujui ni mtu wa aina gani na ana uvumilivu, hekima, utu kiasi gani? Tofauti na uwekezaji mwingine kama wa mali na vitu vingine, mapenzi mnawekeza hisia.

Mnawekeza upendo, ubinadamu, furaha, huzuni kifupi ni maisha kwa ujumla. Uwekezaji wa hisia ni adhimu. Anayekupenda anakuamini asilimia mia.

HUTAMSALITI.

Anaamini mwenye dhamana ya mwili wako ni yeye tu na si mtu mwingine. Anaamini wewe ndiyo msiri wake. Kwamba mnapoishi, unajua mambo yake mengi. Unajua udhaifu wake, unatambua matatizo aliyonayo. Unajua mema na mabaya yake.

Kama ni ugonjwa wewe ndiyo unayeujua vizuri. Kama ni mjuzi wa mambo, wewe ndiyo msiri wake. Kama mzito faragha wewe ndiyo ujuaye. Mnaishi kwa kuchukuliana udhaifu. Mnatunziana siri. Hamzitoi nje kwa sababu nyinyi wote ni wawekezaji. Mmeanzisha taasisi yenu ambayo inawategemea nyinyi ili iweze kustawi.

Mmoja wenu akitoa siri, si kwamba atasababisha mwenzake aadhirike bali mnaadhirika wote. Ndiyo maana kwa mtu yeyote ambaye ni muelewa, ni vigumu sana kutoa siri za ndani hata kama zina fanya hivyo si kwamba atapata ahueni bali watapata fedheha wote wawili kwa mambo yao kujulikana na kila mtu.

Rafiki yangu, unapokuwa kwenye uhusiano na mtu unapaswa kutambua kwamba, amekuamini. Mwenzako ameona wewe unafaa kuwa msiri wake. Amejenga imani kwako. Anakupa thamani kwamba wewe ni uhai wake. Kwa kiwango ambacho yeye anakuamini, nawe pia wapaswa kumuamini hivyo hivyo.

Hayo ndiyo maisha ya uhusiano. Mnajenga imani mioyoni mwenu. Mwanamke amuamini mwanaume, mwanaume amuamini mwanamke. Asitokee mmoja wenu akawa hana imani na mwenzake. Asitokee mmoja akawa na manung’uniko kwa mwenzake.

Inapotokea hivyo, ni vyema mkaweka hoja mezani na kuona namna ya kuondoa manung’uniko hayo. Yawezekana ikawa ni hisia mbaya. Yawezekana ukawa tu ni wasiwasi alionao, mkiyazungumza mtayamaliza na mtaenda sawa. Kwenye uwekezaji wa uhusiano, mnapaswa kuwa sawa.

Asiwepo mtu wa kujiona ni muhimu kuliko mwenzake. Usijione wewe ni bora kuliko mwenzako. Usithubutu kumpa penzi mwenzako eti kwa kumsaidia. Unamsaidia kuwa naye, nani kasema? Uhusiano mzuri ni ule wenye usawa. Hamsaidiani bali mnatengeneza taasisi yenu itakayokuwa na mafanikio.

Ikifanikiwa, mtajivunia na ikifeli basi mtakuwa mmefeli wote. Sasa mnakubali kufeli au kufaulu pamoja? Uamuzi unabaki kuwa chini yenu nyinyi wawili. Mnapoamua kuwa kwenye uhusiano, maisha ya ‘u-mimi’ hayana tena nafasi. Unapaswa kumfi kiria mwenzako ikiwezekana mara mbili zaidi ya vile unavyojifi kiria wewe. Unapaswa kuguswa na tatizo la mwenzako kama vile lkwako.

Naye pia, aguswe kama wewe unavyoguswa. Asipofanya hivyo, kwa kuwa mnajenga nyumba moja basi mnapaswa kukumbushana. Kuelimishana kwa lugha rafi ki na si kufokeana maana hapo hamtajenga bali mtakuwa mnabomoa. Wekezeni upendo kati yenu.

Mwenzako akupende nawe mpende pia. Mjali, naye akujali. Mthamini naye akuthamini, huo ndiyo uwekezaji wa mapenzi. Msiwe pamoja kwenye furaha tu, muwe pamoja katika shida na raha. Mchague kuishi maisha yenu. Muamue kusaidiana, muishi kama marafi ki mnaoweza kukosoana na kurekebishana kwa nia njema na mwisho wa siku uwekezaji wenu utafanikiwa. Mimi na wewe ni mashahidi.

Kuna matukio mengi ambayo yanatokea kwa kukosekana uwekezaji wa mapenzi. Wapo wanaoishi katika migogoro ya kila kukicha. Wapo wanaokosa imani na wenzi wao kiasi cha kutokula chakula wanachoandaliwa, hawaaminiani. Ni hatari kuishi na mtu ambaye haumuamini. Shughulikia tatizo na kama unaona ni kubwa na haliwezekani kusuluhisha basi ni vyema ukavunja uwekezaji.

Ni vyema pia ukawa makini wakati wa kuanzisha uwekezaji. Jiridhishe mara mbilimbili ndipo ufanye uamuzi. Pima nidhamu, hekima busara. Asiwe mtu mwenye historia mbaya. Awe mtu mwenye hofu ya Mungu. Tukutane wiki ijayo kwa

Leave A Reply