The House of Favourite Newspapers

SHOGA; Usikubali Ukoko Siyo Chakula

0

Na SOPHIA MAM`DOGO| GAZETI LA UWAZI| MAKALA

HEEE heeeiyaaa shoga yangu wa ukweli, ni Jumanne nyingine tumekutana kwenye kona yetu hii ya mambo yetu yaleeee, mambo ya mashamsham, mambo ya mahabati, mambo ya kujiachia kama siyo kuelimika, u hali gani shoga yangu?

Najua umesherehekea Sikukuu ya Pasaka vizuri na familia yako, kwa upande wangu nipo vizuri shoga maana mjini kujuliana hali ati! Ila kama mgonjwa ni jambo tu la kuombeana kwa Muumba utapona. Shoga wiki iliyopita nilikushtua kidogo wewe ambaye ulikuwa umejisahau kwa mzee wako, wewe uliyekuwa hujui mzee wako anapenda nini katika chakula cha usiku maana siyo kwa kukaa kaa huko shoga yangu mara mzee anakula chakula kidogo chali, ameshiba, heee heeeiyaa! Mbooona!

Tena utakuta wengine hawajui hata kutenga hicho chakula. Akichakifunua tu anajua kukimbilia kula bila kujua kunatakiwa maandalizi ya kunawa maji na mengine yawepo, umenipata shoga? Baada ya hayo shoga yangu nikulete kwa hiki ambacho kimenikera kama siyo kunichefua.

Hivi kumbe kuna watu wengine bado wanaendeleza vitu vya kuiga Wazungu, loooh! Basi shoga yangu acha nikung’ate sikio maana mibna wewe tenaa, hilo! Kuna msomaji wangu alinitumia meseji nikamjibu na kumpa mbinu, alifurahi sana na kuniomba niliweke wazi ili na wewe shoga yangu unayenisoma hapa upate elimu kutoka kwangu, umenipata somo!

Meseji yake ilikuwa hivi;

“Habari shoga! Pole kwa majukumu ya kuelimisha jamii kupitia kona yako hii. Kiukweli najifunza mengi shoga yangu lakini kuna kitu kimenifanya nishee na wewe pia na wasomaji wote wa kona hii.

“Shoga mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka miwili. Sijaolewa ila natambulika kwa wazazi wa mwanaume ninayeishi naye. Kilichonisukuma shoga yangu hadi kufika hapa ni tabia ambayo mume wangu ameanza kuwa nayo.

“Shoga, mume wangu amebadilika sana siku hizi. Kila tunapofikia muda wa kula chakula cha usiku nakosa raha kwani hunilazimisha nimpe ukoko na mimi sitaki. Nimejaribu kumkatalia lakini hataki na sasa amesema ataenda kwa wengine wanaoweza kumpa chakula kisafi na ukoko wake na kwamba ndiyo atakaowaoa siyo mimi ninayemkatalia. Nimeumia sana shoga kwani bado nampenda sana naogopa hadi kuwaambia ndugu zake!”

Kama ulivyosoma hiyo meseji shoga yangu maana sijataka kuweka nukta wala kutoa koma, upo! Shoga kama nilivyokujibu na kukupongeza kwa ujasiri wako wa kumkatalia katu maana ukoko una madhara makubwa kwa afya ya binadamu, umenipata!

Sasa nakugeukia wewe shoga yangu ambaye nawe umekuwa ukilazimishwa upike chakula chenye ukoko na kumpakulia na ukokowake ama umeshawahi kujaribu kula na mzee. Shoga ukoko una madhara makubwa, kwanza ni uchafu tena uchafu ule unaonuka wa mtaroni, utakubalije kula chakula kisafi kichanganywe na ukoko?

Madhara mengine shoga yangu, ni kupata magonjwa mengi yatakayo hatarisha maisha yako, kumbuka shoga yangu wazee hawa hulazimisha kula ukoko bila kunawa mikono hivyomagonjwa lazima yatatokea kwako na kwake.

Kingine shoga yangu, ukoko husababisha matatizo hata kwa uzao wako ujao nadhani kwa hili umenielewa nisiwe mtoa mifano sana, upo! Kwa leo niishie hapa shoga, tukutane tena Jumanne ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi.

 

Leave A Reply