Sanchez, Ozil Wafanya Kweli, Wafufua Matumaini Ya Arsenal

Wachezaji wa timu ya Arsenal na Middlesbrough wakipambana kuwania mpira, Mpaka mwisho wa mchezo Arsenal walishinda bao 2-0 katika Uwanja wa Riverside Stadium.

Mashabiki wa Arsenal wakiwa na mabango ya kumuondoa Kocha wao Wenger, wakidai mabadiliko.

Mesut Oezil akifunga bao dakika ya 72 kipindi cha pili.

Mesut Oezil akishangilia baada ya kushinda.

Alexis Sanchez akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa timu yake katika dakika ya 42.

Mshambuliaji Mesut Ozil ameendelea kuweka hai matumaini ya Arsenal kumaliza Ligi Kuu ya England ikiwa katika nafasi ne za juu baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wa timu yake dhidi ya Middlesbrough.

Arsenal imepata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo wa ligi hiyo maarufu kwa jina la Premier League, uliopigwa jana usiku.

Mjerumani huyo alifunga bao katika dakika ya 71 baada ya Alexis Sanchez kutangulia kufunga bao la kwanza kwa timu yake katika dakika ya 42.

Licha ya Arsenal kutangulia kufunga bao, wapinzani wao walisawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Álvaro Negredo.

Kutokana na ushindi huo Arsenal sasa ipo nafasi ya sita ikiwa ni nyuma kwa pointi saba dhidi ya timu inayoshika nafasi ya nne, Manchester City lakini City ikiwa imecheza mchezo mmoja zaidi.

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment