The House of Favourite Newspapers

Kutana na Kijana Anayetafuna Chupa na Misumari

0

KIJANA mmoja aliyejitambulisha kwa jina la James John mkazi wa Mchikichini jijini Dar es Salaam ameonakana kuwashangaza watu wengi wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kuwa kivutio kikubwa kwao alipoonekana  akitafuna vitu vya ajabu vikiwemo vipande vya chupa na misumari.

Mtandao huu ulipata fursa ya kuzungumza na kijana huyo ambaye alieleza kuwa yeye ni mzaliwa wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kogoma na alikuja jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupanua uwezo wa kipaji chake cha sanaa.

…Akilimeza betri hilo.

Ameeleza kuwa katika sanaa yake anao uwezo mkubwa wa kufanya vitu vya ajabu vinavyoweza kushangaza watu kiasi cha  kutokuamini kile anachokifanya.  Miongoni mwa matukio yaliyoshuhudiwa na kamera yetu ni  kutafuna vipande vya chupa, kulalia kibao chenye misumari bila kumchoma na kutafuna misumari.

James John akiwaonyesha mashuhuda betri la redio kabla ya kulitafuna na Watu wakimshangilia.

Mbali na hayo,  kijana huyo ameeleza kuwa pia anayo staili ya kubadilisha mkanda kuwa nyoka na kunywa maji lita 20 papohapo.

Baadhi ya wananchi wakimkagua mdomoni kama kweli amemeza msumari.

Katika kuonyesha shoo yake,  hutoza kiasi cha Sh. 100 na kuendelea kulingana na wananchi wanachomchangia.

James akitafuna msumari.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply