Thabit Abdul Atunzwa Mzinga Jukwaani

Thabit Abdul ‘Mtoto wa Ilala’.

AMA kweli kwenye burudani kuna mambo, Jumapili iliyopita ambayo ilikuwa ni Sikukuu ya Pasaka, kiongozi wa Kundi la Wakali Wao Modern Taarab, Thabit Abdul ‘Mtoto wa Ilala’ alijikuta akitunzwa mzinga wa pombe kali badala ya pesa kama ilivyozoeleka.

Shabiki huyo alimtunza Thabiti mzinga huo baada ya kukunwa na sauti ya kinanda kilichokuwa kikipapaswa na mkali huyo kwenye onesho la kundi hilo lililofanyika Ukumbi wa Nefaland uliopo Manzese jijini Dar.

Katika tukio hilo shabiki huyo baada ya kukunwa alionekana kubanjuka kimadaha kisha akamtuma mhudumu akamletee mzinga wa ‘nyagi’ na kumtunza mpiga kinanda huyo mahiri ambaye naye alionekana kuupokea kwa heshima kubwa.

 

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment