Maonyesho ya ‘Harusi Trade Fair’ Kufanyika Mei Dar

 Meneja wa Kampuni ya 361 Degrees, Hamis Omary (kushoto) na kulia ni Naomi Godwin wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na udhamini wao katika maonyesho hayo.

Meneja Biashara wa kampuni hiyo, Hamis Omary (katikati) akizungumza na wanahabari mkutano ukiendelea.

Kaimu Meneja wa Hoteli ya Golden Tulip, Adele Johnson, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na udhamini wao katika maonyesho hayo.

NA DENIS MTIMA/GPL

MAONYESHO ya Tisa yajulikanyo kama “ Harusi  Trade Fair’ yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 3 mwaka huu kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Maonyesho hayo yatakuwa na lengo la kuwapatia maharusi watarajiwa uwanja wa kuchagua mahitaji yao yote wakati wakitarajia kufunga harusi zao.

Akizungumza na wanahabri  jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara wa kampuni ya 361 Degrees ya hapa nchini, Hamis Omary,  alisema maonyesho hayo yatakuwa ya kipekee kwa Afrika Mashariki na hufanyika mara moja kila mwaka.

“Tunapenda kuujulisha umma wa Watanzania kwamba watarajie maonyesho ya kuvutia na ya kuburudisha kwa bwana na bibi harusi kuandaa vitu vyao vya harusi,  pia kutakuwa na mitindo mipya mbalimbali kutoka kwa wauzaji,” alisema.

Toa comment