Mahakama Yatoa Amri Masogange Atiwe Mbaroni - Global Publishers


Imewekwa na on April 21st, 2017 , 10:46:19am

Mahakama Yatoa Amri Masogange Atiwe Mbaroni


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili.
Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo.
Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.
Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa.
 
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya heroin(Diacety Imophine). Pia inadaiwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya oxazepam.
Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Be the first to comment on "Mahakama Yatoa Amri Masogange Atiwe Mbaroni"

Leave a comment