The House of Favourite Newspapers

Tajiri Ammwaga Mrembo Kisa Hawezi Kuzaa

0
Tajiri Sir Benjamin Slade (70).

TAJIRI Sir Benjamin Slade (70) aliyemchukua kwa mbwembwe nyingi mrembo mmoja mfanyabiashara, Bridget Convey, wote wakiwa raia wa Uingereza, hivi karibuni alimbwagilia mbali mrembo huyo akidai kwamba ni mzee mno kiasi kwamba hawezi kuzaa watoto. Milionea huyo hivi sasa anaendesha usaili ili aweze kupata mwanamke anayemtaka.

Benjamin na Bridget Convey.

“Ni mzee mno hawezi kuzaa watoto. Bado tuko marafi ki, lakini hatuko pamoja. Hivi sasa amepata mchumba mwenye umri wa miaka 46 aitwaye Alister Robens,” alisema milionea huyo.

“Mpenzi wangu wa mwisho, Kirsten Hughes, alichukuliwa na fundi wangu aliyekuwa akifanya ukarabati nyumbani kwangu mwaka 2011, lakini naye alikuwa tayari anaonyesha alama za uchizi,” aliongeza tajiri huyo mzee ambaye pamoja na kuchukua na kuacha wanawake wengi, anaendelea na mazoezi na chakula chenye kumwezesha kuwa na nguvu na mwili mzuri katika umri wake.

Leave A Reply