Mtifuano wa Kombe la Shirikisho la Azam leo umefikia patamu baada timu zitakazomenyana katika nusu fainali kujulikana baada ya droo iliyofanyika ofisi za uzalishaji za Azam Media zilizopo Tabata jijini Dar.
Katika droo hiyo Simba itakuwa mwenyeji ambapo itapambana na Azam FC Aprili 29 mwaka huu jijini Dar ambapo Yanga itakwenda Mwanza kupambana na Mbao FC watakaouwa wenyeji wa mchezo huo.
Baada ya droo hiyo wawakilishi wa timu hizo kila mmoja alijinasibu kuonyesha umahiri wake kwenye mchezo huo.
Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati yake ya Utendaji, Said Tuli, Yanga iliwakilishwa na meneja wake, Afidh Saleh, Mbao FC iliwakilishwa na mratibu wa timu hiyo, Masalida Zefania, ambapo Azam iliwakilishwa na Meneja wa timu hiyo, Philip Alando.
(PICHA/ HABARI: RICHARD BUKOS / GPL)