The House of Favourite Newspapers

Barcelona Yatangaza Kumuuza Neymar

0
Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar akifanya yake.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Barcelona, Robert Fernandez amezungumzia juu ya suala la timu hiyo kumuuza staa wao, Neymar kisha kufanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala.

Mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala.

Mwezi jana Neymar alielezea nia yake ya kuwa na ndoto ya kucheza katika Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ huku akiwa pia anawaniwa na matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Fernandez amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Santos, hauziki na klabu yao haina mpango huo kwa sasa.

Mkataba wa Neymar wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2021, akiwa analipwa pauni 110,000 kwa wiki.

Leave A Reply