SHABIKI mkubwa wa timu ya soka ya Kauzi ya Tandika jijini Dar es Salaam, Ally Mussa Nalyamba ‘Babu Ally amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuacha ubabaishaji katika suala zima la uendeshaji wa soka hapa nchini.
Babu Ally ambaye ni mlemavu wa macho (haoni) lakini amekuwa akifuatilia kwa kalibu kabisa michuano ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za timu ya za taifa ameyasema hayo leo alipokuwa kuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha michezo cha Spoti Hausi kinachorushwa na TV ya mtandaoni ya Global TV Online.