The House of Favourite Newspapers

14 Waliofariki Kwa Ajali Ya Gari Tarime Wazikwa – Video

Maziko ya pamoja ya watu 14 waliofariki katika ajali Jumanne Novemba 27, 2018 yakifanyika leo katika eneo la Komaswa maarufu kama Kwa-Gachuma lililopo wilayani Tarime.

 

MAZIKO ya pamoja ya watu 14 waliofariki katika ajali Jumanne Novemba 27, 2018  baada ya magari mawili ya abiria aina ya Hiace kugongana katika eneo la Komaswa maarufu kama Kwa-Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara ambapo magari mawili ya abiria aina ya Toyota Hiace yaligongana uso kwa uso na kuteketea kwa moto,  yamefanyika leo katika eneo waliopata ajali na wengine wawili wamechukuliwa na ndugu zao.

…Mazishi yakiendelea.

Maziko hayo yamehudhuriwa na Waziri Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine mbalimbali.

Waziri Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (wa pili kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa tatu kutoka kushoto aliyesimama) wakiweka shada la maua kwenye kaburi na viongozi wengine.

 

Katika maziko hayo Waziri Lugola ametoa onyo kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto  kufuata sheria za usalama barabarani kwa kuwa serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha wanadhibiti ajali kwa kutoa leseni kwa madereva waliosoma na kufaulu vizuri pia kuwepo kwa adhabu kali kwa madereva wazembe.

Wananchi wakiendelea na maziko.
Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni.

Vilevile, Ummy Mwalimu amesema serikali itawahudumia majeruhi wote kwa kutoa gharama za matibabu mpaka watakapopona.

Lugola akisalimia baadhi ya watu waliohudhuria maziko hayo.
Shughuli ya maziko ikiendelea.
Wananchi wakichimba kaburi.
Wananchi wakiwa pembeni ya Toyota Hiace iliyowaka moto.

PICHA: IDDY MUMBA/TARIME -GPL

 

VILIO VYATAWALA: Mazishi ya watu 14 waliofariki ajalini, LUGOLA aongoza!

Comments are closed.