The House of Favourite Newspapers

Meya wa Jiji Dar Azindua Michuano ya Drafti

0
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita (aliyevaa kofia nyeupe) akicheza Bao na mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.
Baadhi ya washiriki wa mchezo huo wakicheza katika mashindano hayo.
Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar, Kiraba Ngibbombi, akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.

NA DENIS MTIMA/GPL

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amezindua mashindano ya Mchezo wa Drafti yanayofanyika katika viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke leo.

Akizungumza mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar, Kiraba Ngibbombi, amesema chama chao kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ofisi na fedha za kuhudumia na usajili wa chama hicho.

Aliomba kuwepo kwa wafadhili, hasa mashindano yajayo, ili angalau waweze kugharamia vyakula na vinywaji kwa wachezaji.

Mgeni Rasmi, Meya wa Jiji, Isaya Mwita amesema mchezo huo ni mzuri, ila unadharaulika na kuahidi kuwasaidia kufanya usajili wa chama chao ili nao ufahamike kama michezo mingine.

Aidha ameahidi kugharamia nauli na chakula kwa mashindano yajayo kwa wachezaji washiriki ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuuthamini mchezo huo.

Naye Mbunge wa Temeke, Adallah Mtolea, amemshukuru Meya kwa kuanzisha mashindano hayo na akawataka wananchi wa jimbo lake kuelekeza nguvu zao katika mchezo wa Drafti.
Katika uzinduzi huo, Meya na Mbunge walicheza michezo mitatu ya kuhamasisha ambapo Mwita alishinda mmoja na miwili mingine wakatoka suluhu.

Mashindano hayo yaliyoanza leo katika viwanja hivyo vya Mwembe-Yanga na yanayotarajiwa kumalizika kesho, yamedhaminiwa na Mstahiki Meya Isaya Mwita.

Mshindi wa kwanza anatarajiwa kushinda shilingi laki mbili (200,000), mshindi wa pili  laki moja (100,000) na mshindi wa tatu shilingi elfu hamsini (50,000). Jumla ya wachezaji 60 wanashiriki kipute hicho.

 

Leave A Reply