Katika kipindi kipya cha maisha yangu katika jiji la  Dar es salam sikuwa na ndugu wala jamaa katika mji huu wenye hali nzito ya hewa na joto kali.

Rafiki yangu mkubwa alikuwa ni Lody Kenzy, aliye kuwa akinitembelea mara kwa mara nyumbani kwangu katika umbile la kibinadamu, nilimzoea sana hata wakati mwingine kusahau kabisa kama niko na jini na kujiona nipo na binadamu mwenzangu.

Niliendesha ufalme huu kwa ari mno, kubwa zaidi katika jamii hii ya kishetani ni kuhakikisha natengeneza mipango kazi yenye kufarakanisha binadamu na kisha kuwavutia katika jamii yetu.

Nilitengeneza mitafaruku mingi ya kisisa ikiwemo ile ya nchi kama Misri na Burundi,

.Vilevile niliingia hadi ndani ya jamii na kutengeneza matabaka makubwa kabisa kati ya masikini na matajiri na kuwafarakanisha katika misingi ya kidini., haikutosha nilitoa kafara nyingi za watu, maelfu ya watu walipoteza maisha yao kwa mtindo  tofauti tofauti na damu na miili yao ilishia kuwa sadaka kwa majini na mashetani.

Sikuwahi kukumbuka tena kama niliwahi kuwa na ndugu ama mpenzi niliye mpenda kwa dhati na kuwa na ndoto nyingi za kimaisha.****

Ilikuwa ni siku ya juma nne, siku ambayo ni kawaida kuwapo na ibada za kishetani katika kasri  lililokuwapo maeneo ya kigamboni.

Kama kawaida ibada, ilifanyika usiku wa saa tano hadi majira ya saa saba usiku.

Watu  walikuwa wakitawanyika baada ya kumaliza ibada ile, wengi wao walikuwa ni matajiri walio ingia katika usafiri wao na kurejea katika makazi yao..ilikuwa ni kawaida kila baada ya ibada kupitia mapendekezo mapya ambayo huwa yanajiandika kimaajabu kabisa katika kitabu kikubwa chenye kuitwa red book, kitabu kilicho kuwa na lugha ambayo hakuna mtu yeyote mwenye kuweza kuzisoma isipo kuwa mimi peke yangu.

Nilifungua kitabu kile, na ukurasa wa mbele nilikutana na kitu kilicho nifanya nistuke kidogo, kulikuwa na mandishi mekundu yaliyo andikwa kwa herufi kubwa, na wino wenye kukolezwa, nilitakiwa kuwaongoza katika tawala hiii ya wajenzi huru viongozi wakubwa hasa wenye ushashiwi na nguvu za kimungu katika jamii zao.

Lakini pia, maandishi yale yalinipa ruhusa ya kumua yeyote endapo kutakuwa na ukinzani mkubwa kutoka kwake.

Yapata  saa sita kasoro nilikuwa ndani ya kivuko cha Mv magogoni, ndani ya BMW magari ya kisasa ambayo ndiyo yalikuwa yanaingia nchini wakati huo, dakika sita zilitosha kuwa ng’ambo ya pili.

Usiku ule hapakuwa na msongamano wa magari, nilikanyaga mafuta na ndani ya nusu saa nyingine zilitosha kunifikisha nyumbani kwangu.

Niliingi ndani ya bangaluu langu la kifahali kuishia ukumbini, huku nikiwa bindamu mwenye furaha kubwa ya maisha.

Nilifungua jokofu kubwa ambalo huwa nahifadhi vinywaji mbali mbali, ni hapo nilipo hisi mabadiliko ndani ya nyumba ile.

Chupa ambayo huwa nahifadhi kinywaji nilicho kifurahia kunywa chupa hiyo haikuwemo ndani ya Jokofu.

Hata nilivyo kuwa nikitahayari hali ile ndipo nilipo hisi uwepo wa binadamu nyuma yangu.

Niligeuka.

Nilikutana macho kwa macho na afande Mwita  aliyekuwa amekamata bastola kubwa iliyo valishwa kifaa chenye

kuzui sauti perfolted sylinder  huku mkono wa kushoto akiwa amekamata chupa iliyokuwa na damu ya bindamu.

“Unatafuta hii Vegasi?” alisema  jamaa kwa kejeli huku akinitizam kwa makini.

“Wewe umeingiaje humu ndani na shida yako nini bwana mdogo?”

“Namna nilivyo ingia humu ndani siyo muhimu kuliko kujua dhamila ya kuwepo humu katika hii pepo yako uliyo jitengenezea hapa duniani.”

“Haya, dhamila yako ni nini bwana askari?” nilimuuliza kwa kejeli.

“Swali zuri, jambo moja tu ninalo taka kwako, roho yako na hii ni kwa ajili ya mchumba wangu Mkami damu yake nimekuja kuilipa sasa.”

“Wee mbona unafurahisha hivyo, huyo mkami nilimua mimi au ulimua mwenyewe.. pili kama umekuja kuchukua roho yangu sasa kinywaji changu cha nini uwe nacho..au wewe pia unatumia vitu hivyo?” niliuliza kwa kejeli.

Afande Mwita alinyanyua Bastola yake na kunielekezea, nikaona unavuta kifytulio cha risasi na hapo mlipuko mdogo sana ukasikika na risasi ikatoka ndani ya bastora yake na kunipiga katika kifua,

MAAJABU!..

Ilikuwa ni kama vile nimepigwa na yai katika kifua changu, sikuhisi chochote katika mwili wangu, risasi ile ilidunda na kuanguka chini, jamaa alibabaika, akanifyatulia risasi nyingi mwilini mwangu, lakini mwili wangu nilikuwa kama roboti hakuna risasi hata moja iliyopenya katika nyama.

Hatimae Risasi zote ziliisha katika bunduki yake, nilitabasamu kwa kejeli, huku nikimtizama yule mtu mwenye chuki kubwa ya kisasi.

“Bado unahitaji kucheza na mimi Mwita?” nilisema nikimtizama, niliona mashaka makubwa mno kwa mtu yule, hakuwahi kutegemea kukutana na kiumbe kama mimi kamwe.

“Wewe ni jini, wewe?” alisema huku akirudi nyuma kamasi likimtoka puani mwake macho ya hofu yamemtoka.

“Jini siyo huyo,.. jini ni mimi” sauti nyingine ilitokea nyuma yake, Lody Kenzy alikuwa ametokea katika umbile lake, la kijini akiwa mwingi wa hasira.

Afande Mwita aligeuka nyuma upesi sauti ilikotokea, na hapo macho yake ya kibinadamu yakaweza kuona kiumbe yule mwenye kutisha vibaya mno, suruali yake ililowa ghafla kwa mkojo ulio mtoka, alitetemeka kama mgonjwa wa degedege.

Macho yamemtoka pomoni, alihema kwa kasi mno, dakika tatu zilikuwa nyingi kuweza kumfanya afande Mwita aendele kuwa katika uhai, alikufa kwa shinikizo.

Heri ukutane na mnyama yoyote mkali wa mwituni kuliko kukutana na jini akiwa katika umbile lake lenyewe.

Anatisha.

“Mshenzi huyu, kamua Saumya Kohil” alisema Lody Kenzy akijirudisha katika umbile la kibinadamu.

“Aah!..Nani, Hashim Azizi?” niliuliza kwa mshangao.

“Ndiyo”

Ebwana wee.! Nilishanga zilikuwa ni habari zilizo nisisimua kaisi, kwa mara ya kwanza nikapatwa na masikitiko kwa  mtu yule kupoteza uhai wake kwani nilihisi askari yule kwa kiasi Fulani uchunguzi wake uliweza kumbaini Hashim Azizi ni nani, na hata kumua, ningependa kujua vpi alimbaini Hashim Azizi na hata kumchukualia hatua hiyo ya kifo.

“Vegasi kuna jambo la muhimu ambalo unatakiwa litekelezwe ndani ya masaa arobaini na nane…achana na huyu binadamu jeuli” Alisema Lody Kenzy.

“Jambo lipi hilo?” niliuliza

“Mtu mwenye kuitwa Shekh Othumani Hilal ametoka katika gereza na sasa yupo humu Jijini, chini ya kitaasisi mchwara chenye kuitwa Hizib Ut Tahaliri, watu hawa  wanajitia uwanaharakati wa kishenzi, hivi ninavyo zungumza na wewe, mtu huyu mwenye kutiwa Othumani Hilal, anakiandika kitabu chenye kuelezea  siri na mipango yetu katika dunia.”

“Huyu mtu namfahamu, niliwahi kukutana nae katika Gereza, sasa katoka vipi ilihali alikuwa na kifungo kirefu jela.?”

“Huyu mshenzi aliye lala hapa ndiye alie fuatilia shauri lake upya na mahakama ikaona hana hatia na kuachiwa huru”

“Unataka kuniambia afande Mwita alifuatilia upya kesi ya Othuman Hilal na kuirejesha kesi katika mahakama?”

“Ndio”

“Kwanini alifanya hivyo?”

“Mwita alikuwa akijaribu kufuatilia habari zako kwa ukaribu zaidi ndani ya gereza, na mtu aliye msadia kwa karibu zaidi alikuwa ni huyo mzee ambaye kwa kiasi fulani kama unakumbuka niliwahi kukueleza ndiye mtu aliye wahi kumsaidia mama yako dhidi ya kifo, baada ya  kuzaliwa mwanaume na kufa na kuzaliwa upya akiwa mwanamke.”

Alisema Lody Kezy. Baada ya hapo nilimuhakikishia kabla ya mchana wa siku itakayo fuata Othumani Hilal atakuwa tayari maiti.

******

Nilikuwa ndani ya nyumba ya vyumba sita, huko maeneo ya ilala Boma, ndani ya chumba alicho kuwa akilala Othuman Hilal.

Yapata saa kumi na moja alfajiri, ndani ya chumba kulikuwa kutupu, hapakuwepo na mtu japo nilikusudia kuwa mahala aliko huyu mtu,. nilishanga kidogo kwani haijawahi kutokea pale ninapo nuia kuwa mbele ya kitu ama mtu fulani, kisha niibuke eneo husika huku mtu niliye mkusudia nisimwone!.

Atakuwa wapi huyu mtu, ndani ya chumba hicho kulikuwa na laptop ndogo iliyokuwa imewashwa, hii ilionyesha muhisika aliyekuwa mule ndani hakuwa mbali na mazingira yale ya mule ndani.

Nilichunguza ile laptop ndogo nikaona maandishi mengi, na hata nilipo soma aya kadhaa katika yale maandishi nikagundua kazi aliyo kuwa akiifanya Shekh Othumani Hilal ya kuandika kitabu chenye kufichua siri za utawala wetu ndio hicho.

Kwa nguvu za giza nilihalibu kabisa harddisk ya mashine  ile kwa kuiuwa kabisa.

Wakati huo huo, nilisikia sauti za watu waliokuwa wakiingia humo ndani. nilijiweka tayari kwa vita, watu watatu walio valia kanzu nyeupe walingia mule ndani, mmoja wao akiwa ni Shekh Othumani Hilal, walionekana ni watu walio toka musikitini majira yale ya asubuhi.

Macho yake yalishia katika laptop yake iliyo kuwa tayari imezima baada ya kufanya ule uhalibifu.

Aliiwasha lakini harddisk ilikuwa imepoteza kumbukumbu zote huku yenyewe ikiwa imekufa.

Nilimwona namna Shekh Othuman alivyo haha, alipata mfadhaiko mkubwa kwa kupoteza kazi muhimu kama ile ambayo bila shaka alitumia akili na nguvu nyingi kuitengeneza.

Nikiwa nimesimama pembeni yao, pasina wao kuwa na uwezo wa kuniona, nilizungumza maneno fulani ya kichawi, na hapo, mara shekh Otumani Hilal alipatwa na kichwa cha ghafla.

“Kwisha habari yako” nilisema moyoni na kuondoka taratibu mule ndani nikimuacha mzee yule akigumia maaumivu makali ya kichwa  ambayo asingiweza kumaliza hata risaa limoja akiwa bado yupo hai.

Nilitoka nje ya nyumba ile na kuchukua usawa wa barabara ya kuelekea magomeni tayari kwa kurejea nyumbani kwangu.

Mara hiyo hiyo Lody Kenzy alinitumia ujumbe kichwani na kuniambia kuwa sijamaliza kazi natakiwa nirudi  nyuma na kuhakikisha mzee yule ameondoka kabisa duniani.

Nilirudi katika nyumba ile, sasa hivi nikienda katika hali  ya kuweza kuonekana katika macho ya binadamu.

Ngo ngo ngo, nilibisha hodi mlangoni, katika nyumba ile aliyoishi Shekh Othumani Hilal na wenzake.

Ngo ngo ngo. Nilirudia tena kugonga na mara kitasa cha mlango kikanyongwa kulia na kushoto kisha mlango ukafunguliwa.,

Sikuamini macho yangu kwa kile nilicho kiona.

Shekh Othumani Hilal alisimama wima mbele yangu, akiwa mwingi wa afya njema, kama kwamba hakupatwa na aina yoyote ya kadhia muda mchache uliopita.

“Weee!!. VEGASI!.” Jamaa aliniita kwa mshangao, akiwa haamini kuniona nyumbani kwake.

Nilibaki pia nimeduwaa nashindwa kuamini mtu huyu kapona vipi kwa uchawi wenye nguvu kubwa kabisa nilio mtumia.

Basi ikawa ni taharuki mtindo mmoja, yeye akishangaa uwepo wangu pale huku mimi pia nikimshanga vipi mtu huyu andelee kuwa hai.

Nilipita ndani huku bado nikiwa nausaili mwili wa yule mtu ambao haukuonyesha kuathilika na uchawi mkubwa kama ule.

“Umependeza haswaa! Waashi wapi na vipi uwe huku? Umepajuaje hapa” yule mzee alikuwa na maswali mengi ambayo aliyauliza bila mpangilio, ikawa akinitizama mavazi yangu ghali niliyo kuwa nimevaa mwilini mwangu.

“Humu humu Jijini mzee, vpi wewe mzima?”

“Mie mzima, karibu tafadhali” alisema na kunikaribisha katika zuria kubwa katika ukumbi mkubwa usiyo kuwa na viti.

Pale walikuwa wameketi wale jamaa wawili walio onekana kama ma-Ostadh, walikuwa wakisoma Qurani kwa sauti,

“Karibu ndugu yangu, karibu sana” alinikaribisha zaidi mzee yule kwa ukarimu mkubwa kabisa.

Wakati naketi chini, sikuhitaji kupoteza muda  palepale nilinuia uchawi mwingine mkubwa kabisa ambao ungemwondosha mtu yule kwa dakika kumi tu.

Wakati huo mzee huyo Othumani Hilal, alikuwa amekamatia tasbihi yake mkononi akiwa kama anahesabu vitu fulani  kimoyo moyo. Huku akiwa tayari  kunisikiliza kwa kile kilicho nileta.

“Ndiyo bwana” alisema, katika namna ya kusikiliza ujio wangu.

Uchawi nilio utuma kwa mtu huyo usiyonyeshe matokeo yoyote,

“Ndiyo bwana Vegasi, kulikoni?” aliuliza tena, baada ya kuniona nipo kimya, mara hiyo hiyo nilihisi nafinywa kwa nguvu nyingi na kitu fulani mwilini mwangu,         `

Sikujua vipi hali ile inatokea, pengine wale jamaa walikuwa na uchawi mkubwa wenye kuushinda ule wangu, lakini vipi  hili liwezekane hili. Na kadiri sekunde zilivyo zidi kuyoyoma ndivyo nilivyo zidi kufinywa kwa nguvu mwilini mwangu, nilikunja uso kama nimekula shubiri, wale jamaa mule ndani nikaona namna wanavyo patwa na mshangao ghafla kutokana na mabadiliko yangu, “vipi una tatizo gani kijana?”  aliuliza shekh Othuman, hapo hapo nilijikuta nikitoa yowe kubwa, lililowafanya jamaa wapatwe na mashaka makubwa mno.

Ilikuwa ni kama  nachomwa chomwa na kingingi cha moto, maumimvu makali yalinitambaa mwilini mwangu.

Ajabu ni kuwa yule mzee niliye mloga yeye alibaki kuwa katika hali ya kawaida kabisa, wakati huo huo nnilihisi macho yangu yakipoteza uwezo wa kuona na kugubikwa na giza zito.

Ndani ya giza hilo nilihisi taswira ya viumbe wa ajabu ajabu wakipita mbele ya macho yangu, nukta kadhaa nikiwa katika hali mbaya ya maumivu ambayo hayamithiliki, nilihisi kukabwa  shingoni na  kwa nguvu na kiumbe aliye jitokeza katika namna ya upepo mkali mbele yangu.

Dhamila ya kiumbe yule ni kuniua kwakuwa nimekuwa dhaifu kwa viumbe waliotokana na tone ama majimaji dhaifu yatokayo katika viungo vya uzazi wa mwana wa Adamu, wewe umeubwa kwa moto, unashindwa  na viumbe hawa?? Sasa lazma ufe wewe, ili kulinda siri za ufalme wetu

Kiumbe yule kiumbe  alikoroma kwa ukali, pumzi zilikuwa zikinishia, na  sasa niliona naenda kuzimu.

Lakini wakati huo huo nilihisi kuguswa kichwani na kisha nikasikia maneno fulani ambayo sikuyaelewa lugha yake, maneno yale yalikuwa yakizidisha hasira kali kwa yule kiumbe aliyenikaba shingoni na kuongeza nguvu zaidi ili nife haraka, giza lilikuwa zito zaidi machoni mwangu

*******

Zaidi ya dakika kumi na tano nilikuwa nimepoteza fahamu, kope za macho yangu zilifunguka taratibu na kukuta nimezungukwa na watu takriabni kumi waliokuwa wamenyanyua viganja vya mikono yao usawa wa vifua vyao, wakiwa ni wenye kusoma Dua, hakuna aliye onekana kujali kwa kuamka kwangu, wote walikuwa wamezama katika maombi mazito kabisa, nilikuwa nikihema, huku nikajiribu kufikiri kitu kilicho tokea.

Dakika tatu badae  jamaa wakihitimisha kwa kunisomea moja ya aya kuu katika Quran ambayo nilikuwa nikiifahamu enzi hizo kabla ya ‘kulunduka’na kuwa kiumbe wa ajabu.

Walirudia rudia yale maneno yaliyo nifanya nijitapikie vibaya mno na kutoa vitu vya ajabu kabisa tumboni mwangu,.

Mtu mmoja alisafisha eneo lile nililo tapika kisha kila mtu akawa tayari kusikia juu ya maswahibu yanayo nisumbua.

Lakini kabla ya kuzungumza, Othuman Hilal alianza kutoa hadithi vile alivyo nifahamu mimi,  hakusita kuzungumza kuwa hata matokeo ya yeye kuwa huru ni baaada ya kutoa ushirikiano mkubwa kwa askari mpepelezi aliyekuwa akifuatilia kesi iliyokuwa ikimkabili. Shukrani kubwa ya askari yule ilikuwa ni kurejesha shauri lake katika mahakama na kumtafutia wanasheria wazuri, na kesi yake kusikilizwa upya, kabla ya  yeye kukutwa hana hatia Dhidi ya tuhuma zilizo muweka gerezani kwa zaidi ya miaka kumi.

Sikujua nianzie wapi kuzungumza dhidi ya yale yaliyo nipata katika maisha yangu, hata wakati huo mwili wangu ulikuwa dhaifu mno, nilikuwa ni kama nimetua mzigo mkubwa ulio kuwa mwilini mwangu, sikuwa na nguvu za kichawi tena, niliomba muda wa kupumzika kabla ya kutoa  hadithi ya maswahibu yaliyo nifika katika maisha.

Wale watu walikuwa ni watu wema wenye hekima, hakuna aliye tia neno, ila kabla ya kupumzika, nililetewa maji yaliyo kuwa na  rangi ya njano, na kutakiwa kunywa huku nikiambiwa maji yale  ni maji yaliyo changanywa na wino mbichi ulio kuwa umendikiwa maneno matakatifu ya mwenyezi Mungu {kombe}.

Hata nilipotwaa yale maji nilijihisi kuwa  na nguvu kabisa, ule unyonge niliokuwa nao mwilini ulitoweka ghafla.

Nilipata zaidi ya masaa sita ya kupumzika mule ndani, nililala katika moja ya vyumba katika nyumba ile.

Baada ya maaasa zaidi ya saba niliamshwa na  Shekh Otumani Hilal kwa ajili ya kujianda kwa kwenda katika ibada.

Nilioga vema kupewa kanzu nzuri nyeupe kisha tukaongozana na mzee yule hadi katika musikiti mkubwa wa ijuma pale Ilala Boma.

Nikiwa njiani kuelekea katika ibada kwa mara ya kwanza nilijona ni binadamu ninaye nuka dhambi.

Kwa hakika nilikuwa nimemuasi Mungu wangu kwa kiwango kikubwa kabisa nilihitaji toba ya kweli na dhati.

Tulipo ingia ndani ya Musikiti ule, nikiwa katika eneo la kujisafisha {udhu} nilimwomba Shekh Othumani Hilal kutangaza kile kilicho tokea katika maisha yangu ndani ya musikiti ule wenye kuingia watu wengi.

Nilihitaji kuiambia dunia nzima uovu na mbinu za ibirisi kwa wadamu.

Baada ya ibada ile iliyo endeshwa na Shekh Othumani Hilal kumalizika, watu walitangaziwa kutoondoka, na kutakiwa kupata  muda na kusikiliza mkasa wa kweli ulionikuta, mkasa  wenye funzo kubwa kabisa katika mambo ya imani na uchaMungu.

******

Mwaka mmoja badae, nilikuwa bidamu niliye ishi kwa furaha, amani na tumaini la kweli, sikuwahi kutokewa na jini wala ndoto yoyote isiyo ya kawaida.

Niilishi maisha ya kichamungu nikiwa mswalihina haswaa nisiye pitwa na kipindi hata kimoja cha ibada.

Sasa ni kijana wa umri wa miaka thelathini na tano, nina watoto wawili, wa kwanza wa kiume mwenye kuitwa  Hussein na wapili ni wakike mwenye kutwa Khadija.

Mke mzuri, mchamungu na mshauri mwema, mwenyeji wa huko unguja kiembe samaki, anaitwa bi Latifa binti Kassim Bakari.

Sambamba na hayo, nakushukuru wewe uliye chukua muda wako na kusoma upuuzi wangu, ambao kwa upande mwingine ni funzo kwako…

Asante sana.

TAMATI.

Toa comment