The House of Favourite Newspapers

Video: Mecky Mexime, Masau Bwire Wafunguka Mazito Ndani ya Sport House

0
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime (wa pili kutoka kushoto) akiwa na watangazaji wa kipindi cha  Sport House   kutoka kulia ni Saleh Ally Saleh, Wilbert Moland na Philip Nkini (kushoto).
Wakiendelea na kipindi.

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime  kupitia kipindi cha Sport Housi cha Global TV Online leo amesema kuwa ujio wa kipa mkongwe, Juma Kaseja kwenye usajili wa dirisha dogo ulikiimarisha kikosi chake na kusababisha kumaliza Ligi Kuu Bara katika nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Maxime aliongeza , mshambuliaji Ame Ally na Fakhi waliotua kwenye usajili huo wakitokea Simba nao walitoa mchango mkubwa katika timu hiyo na kuiwezesha Kagera kumaliza kwenye nafasi hiyo ya tatu.

Naye Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amekanusha taarifa zilizoonea kuwa ni yeye shabiki wa Simba.

“Niseme tu, Simba, Yanga na Azam FC zilinifuata kwa ajili ya kufanya kazi ya usemaji kwenye timu zao na nikakataa, halafu niwaambie wadau wa soka kuwa mimi siyo shabiki wa Simba,”alisema Bwire.

Bwire Msemaji mwenye maneno mengi wa Ruvu Shooting, Masau Bwire akifunguka ndani ya kipindi cha Sport House.

…Wakiendelea na kipindi.


Leave A Reply