The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege la Etihad Lasherehekea Kuwasili Kwa Ndege Yake ya 10 Aina ya A380

0

NDEGE ya 10 na ya mwisho aina ya Airbus A380 ya Shirika la Ndege la Etihad imewasili.

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Etihad walijumuika pamoja katika Uwanja wa Ndege wa Hamburg Finkenwerder nchini Ujerumani barani Ulaya ambapo ndege hiyo ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa shirika la ndege la uarabuni kabla ya kuanza safari zake za uwasilishaji nchini Abu Dhabi.

Ndege za aina ya A380s zilizojishindia tuzo kadhaa, ni ndege za kibiashara zenye utofauti wa kipekee kwenye huduma zao kama malazi –vyumba vitatu vyenye ukubwa wa kuweza kuishi watu mpaka wawili vikiwa na sebule, bafu binafsi na chumba cha kulalia. Ndege hizi pia zinajivunia kuwa na “appartments” 9, studio za biashara 70, mahala pa kupumzikia na siti nzuri 415 kwenye daraja la uchumi.


Ndege ya Etihad A380s inatoa huduma kutokea nchi za uarabuni kwenda Mji Mkuu wa London, Sydney, New York na kuanzia tarehe 01/07/2017 watakua Paris.

KUHUSU SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.
Shirika limewekeza kwenye mashirika saba; : Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya chini ya Etihad.
Makao makuu yake yakiwa Abu Dhabi, Shirika la Etihad limetangaza malengo ya kuhudumia abiria 117 na mizigo Mashariki ya KATI, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boing 122, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa; ikiwamo 71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s and 10 Airbus A380s.Tembelea: www.etihad.com

Leave A Reply