The House of Favourite Newspapers

Azam Yamshusha Dar Mchekeshaji wa Uganda, Teacher Mpamire

0
Mchekeshaji namba moja kutoka Uganda, Teacher Mpamire muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Julius Nyerere.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vipindi na televisheni ya Azam Media leo imemshusha mchekeshaji mashuhuri kutoka nchini Uganda, Teacher Mpamire ambaye anatarajiwa kuwaburudisha mashabiki kwenye tamasha la Sikukuu ya Eid Mosi linalotambulika kama Eid Comedy Gala.

Mchekeshaji huyo anatarajiwa kuwa sambamba na wasanii wengine wa Kibongo kama vile MC Pilipili, Dogo pepe, Mau Fundi na Katarina wa Karatu.

Mbali na mchekeshaji huo, mchekeshaji mwingine kutoka nchini Kenya, Eric Omond naye anatarajia kutua Dar kesho.

Wafanyakazi wa Azam Media wakimpokea Teacher Mpamire.

Akizungumza na Mtandao huu juu ya ujio wa mchekeshaji huyo, Mratibu wa Eid Comedy Gala, Yahya Mohamed amesema kuwa mashabiki watarajie kupata burudani za kutosha kutoka kwa wakali hao walioshindikana kwenye kuvunja mbavu na kwamba shoo hiyo itawawezesha wasanii wa hapa nchini kubadilishana mbinu mbalimbali za kiuchekeshaji na ujuzi mbalimbali.

“Eid Comedy Gala ni moja kati ya matamasha bora na la kwanza kufanyika nchini Tanzania likiwashirikisha wakali wengi kutoka Afrika Mashariki. Niwaombe wapenzi wote waje kwa wingi kuvunja mbavu zao. Pia itakuwa fursa kwa wachekeshaji kukutana na kubadilishana mawili matatu,” alisema Yahya.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar es Salaam Sikukuu ya Eid Mosi.

Picha/Habari: Denis Mtima

Leave A Reply