The House of Favourite Newspapers

Droo Ndogo ya 5 ya Shinda Nyumba… Wasomaji wa AMANI Wapagawa

0
Mshindi wa pikipiki droo ya nne akiwa na mkewe baada ya kukabidhiwa zawadi.

 

WAKATI Droo Ndogo ya Tano ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ikiendelea kubamba kila kona ya nchi, wasomaji wa Gazeti Amani ambalo ni moja kati ya magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers, wameonekana kupagawishwa baada ya kunaswa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar wakilinunua kwa kasi, lengo likiwa ni kujishindia zawadi mbalimbali.

Fadhili Mkuru akisoma Gazeti la Amani baada ya kujaza na kukata kuponi ya Shinda Nyuba

 

Mr. Shinda Nyumba aliyekuwa kwenye mishemishe za kuitangaza bahati nasibu hiyo ndiye aliyewabamba wasomaji hao Alhamisi iliyopita maeneo ya Mbagala wakinunua gazeti hilo na kujaza kuponi zilizokuwa ndani ili waibuke washindi.

 

Jackson Kiluwasha wa Mbagala akijaza kuponi ya Shinda Nyumba katika Gazeti la Amani akiwa ndani ya daladala yake

 

Wakati hayo yakiendelea, taarifa nyingine nzuri ni kwamba zawadi kibao zikiwemo pikipiki, simu, Dinner Set, TV na nyinginezo zinatarajiwa kutolewa kwenye droo ndogo ya tano inayotarajiwa kuchezeshwa Julai 20, mwaka huu.

 

Mafundi magari kutoka Mbagala wakiwa katika picha ya pamoja na Mr. Shinda Nyumba baada ya kununua Gazeti la Amani na kujaza kuponi ya Shinda Nyumba

 

Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Amani, Uwazi, Risasi na Ijumaa Wikienda, Yohana Mkanda amesema mahali ambapo shughuli hiyo itafanyika itafahamika siku chache zijazo.

Mathayo Oforo wa Mbagara – Rangi Tatu akiwa amenunua Gazeti la Amani tayari kwa kujaza kuponi ya Shinda Nyumba

 

“Ninachoweza kuthibitisha ni kuwa droo hii ya tano itafanyika Julai 20, kuna vitu vidogo tunavifanyia kazi ili tuweke wazi mahali ambapo shughuli yetu itafanyika,” alisema Mkanda.

 

Rapa wa ‘Stamina akiwa na Mr Shinda Nyumba

 

Kabla ya droo hiyo ya tano, tayari Global Publishers imeshafanya droo ndogo nne ambazo zilifanyika katika maeneo ya Mbagala Dar Live, Manzese Bakhresa na CCM Mwinjuma Mwananyamala (mara mbili).

 

Suleimani Samir wa Mbagala akiwa na Mr Shinda Nyumba baada ya kununua Gazeti la Amani na kujaza kuponi

 

Katika droo hizo zote, washindi wamekuwa wakipewa zawadi mbalimbali ambazo zimebadili maisha yao, zikiwemo pikipiki, televisheni, simu za kisasa za mikononi, vyombo vya nyumbani na ving’amuzi kutoka Kampuni ya Ving’amuzi vya Ting.

Swaumu Ramadhani wa Mbagala akiwa dukani kwake akijaza kuponi ya Shinda Nyumba katika Gazeti la Amani

“Kwenye magazeti yetu yote, katika kurasa za pili zipo kuponi zenye maelekezo ya namna ya kufanya, ukishamaliza kujaza, unaweza kuzituma kwetu kupitia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima au wale wa Dar wanaweza kuja ofi sini kwetu, Bamaga Mwenge na kuziacha kwenye ndoo ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda wakati akiwaelekeza wasomaji namna ya kujaza kuponi hizo.

Washindi wa droo ya nne wakiwa wamekabidhiwa zawadi zao za ving’amuzi vya Ting

 

Bahati Nasibu hii imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Leave A Reply