The House of Favourite Newspapers

Waziri Wa Fedha Na Mipango, Dkt. Philip Mpango Ajiunga Na PSPF

0
 Waziri Dkt. Mpango (kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.

 

Waziri aliyasema hayo jana Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba wakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.

 

“Mimi nitoe wito kwa wananchi  kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi
muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango. Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

 

“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo
mwananchama” Alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

 

Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari,
kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.
“ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe.Waziri.

 Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF
 Waziri Dkt. Philip Mpango, (kulia), akipokea mkoba wenye vipeperushi vya taarifa mbalimbali za PSPF, kutoka kwa balozi wa Mfuko huo, Msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kutembelea banda la Mfuko huo Julai 8, 2017
 Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliofika kutembelea banda la Mfuko huo
 Bw.Noah Amri, (kulia), Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na mwanchi huyu aliyeshika fomu yakujiunga na Mpango huo
Maafisa wa PSPF wakiwa kazini.
(Picha/Habari: K-VIS BLOG/Khalfan Said)
Leave A Reply