The House of Favourite Newspapers

CHECHE ZA MZEE CHEKECHE, KIJANA WA ZAMANI!

0

CHECHE ZA MZEE CHEKECHE, KIJANA WA ZAMANI!

ANAITWA Chekeche, hana cheti cha kuzaliwa, lakini inaaminika kuwa wakati Vita ya Pili ya Dunia inaendelea, Chekeche alikuwako. Wengine huenda mbali kwa kusema Chekeche alipata miaka sabini na tano, wapo waliotia chumvi kwa kuzusha ati alikuwa kikongwe aliyepata miaka mia moja na mitatu! Chekeche mwenyewe alipoulizwa umri wake, alijibu:

“Im not old, I’m a young man with experience!”

Yeye alipenda kuulizwa maswali ambayo alifurahi kuyajibu. Swali kuhusu umri wake, hakulipenda.

Usiku ule, Mzee Chekeche alikaa kaunta ya juu akiufurahia mvinyo. Alikuwa ndani ya Club ya usiku ya Malibo, sauti mororo ya muziki wa kiulimwengu ilitumbuiza taratibu. Watu wengi walikuwa katika ‘dancefloor’ wakicheza kama mazuzu, huyu kayumba huku, mara kayumba kule, mwingine karuka… walevi walisumbua vilivyo!

Chekeche alikwishakolea kilevi. Hata sharubu zake za kambale zililowa, zikalala usingizi mzito. Sura yake yenye makunyanzi, ilizidi kujikunja maradufu. Alisikika akiropoka kwa nguvu, “Usiku wa leo siwezi kulala peke yangu!” Hapo akaifakamia ‘dancefloor’, harakaharaka akakamata makalio ya dada mmoja aliyekuwa amenogewa muziki, msichana akashtuka kwa furaha, alihisi dalili za kupata mteja.

“Una shingapi?” msichana aliuliza, akimlegezea jicho mzee Chekeche.

“Alfu kumi itakufaa?” alihoji Chekeche.

“Akha babu we! Kwani mi bando la makaratasi? Fanya thelathini!”

“Sawa!” alikubali Chekeche huku akimshika mkono dada yule tayari kuianza safari ya kibiashara! Mlevi mmoja alipowaona, akafyatua maneno:

“Dada umekosa cha kuuza mpaka unajiuza mwenyewe!”

Hawakuyajali maneno hayo, waliendelea na hamsini zao… safari ya kibiashara!

Punde si punde, Chekeche na mwanamke wake, walikuwa ndani ya chumba cha gesti mojawapo iliyokuwa umbali mdogo kutoka ‘Malibo club’. Mzee alimtazama kwa matamanio makubwa dada yule mfanyabiashara ya kuuza mwili. Haraka kama radi akamrukia na kumchojoa nguo zake.… vurugu za hapa na pale, walikuwa kitandani…

Mzee akaichomoa ‘chuchu’ msumari iliyokaa vyema katika kifua cha dada kahaba, akanyonya kama ndama mwenye njaa, kisha baada ya hapo akalala usingizi mzito.

Masikini mzee Chekeche, kumbe alitegwa madawa, basi dada yule kahaba, akapora vyote alivyokuwa navyo mzee!

Mzee Chekeche kapitia mikasa mingi ya kusisimua… kisa chake kingine  kitaruka Jumatano… usikose!

 

Leave A Reply