Sol Campbell Alivyosherehekea Ushindi Wa Arsenal Na Mashabiki Wa Tanzania
Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell, leo aliiangalia mechi ya timu yake hiyo ya zamani ilipokuwa ikimenyana na Chelsea katika mchezo wa kugombea Ngao ya Jamii.
Mchezaji huyo aliuangalia mpambano huo kupitia luninga kubwa kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar sambamba na umati mkubwa wa mashabikii wa timu hiyo hapa nchini. Ulipofika wakati wa mapumziko, mchezaji huyo aliwapa zawadi mashabiki aliowauliza maswali kuhusu historia yake ya soka na kumjibu vizuri.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL