The House of Favourite Newspapers

Jokate Amtamani Rihanna!

0
Mwanamitindo Jokate Mwegelo.

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo amefunguka kuwa pamoja na kukutana na wanamuziki mashuhuri, Shawn Carter ‘Jay Z’, Beyonce Knowles na mchezaji Thiery Henry, mwingine anayetamani kukutana naye maishani ni mwanamuziki Robyn Fenty ‘Rihanna’ pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama na mkewe, Michelle.

Mwanamuziki Rihanna.

Jokate alifunguka hayo juzikati baada kutimiza ndoto yake ya kukutana na mwanamuziki nguli Afrika, Oliver Mtukudzi nchini Afrika Kusini hivyo kuweka wazi kuwa kiu yake imebaki zaidi kwa Rihanna.

“Natamani sana kukutana na mwanamuziki Rihanna pia Obama na mkewe. Rihanna namuelewa sana kwa sababu tunafanana hadi mauombo yetu, itakuwa safi sana nikikutana naye,”alisema Jokate.

 Stori: Gabriel Ng’osha | Amani | Global Publishers

Esha Buheti: Jini Kabula Kweli Anaumwa, Tumsaidieni!

Leave A Reply