The House of Favourite Newspapers

Namba 11 ilivyoliteka tukio la Septemba 11 Marekani

0
septemba 11
Shambulio la Septemba 11 Marekani.

DUNIA ina maajabu yake, mtu unapomwambia kuhusu mfanano uliokuwepo baina ya Rais John F. Kennedy na Abraham Lincoln, anashangaa na kustaajabu. Watu wanashangaa kwa kuwa dunia inashangaza, mpaka leo hii, hakuna mtu anayejua namna mapiramidi ya Misri yalivyojengwa, ni mawe makubwa mno, kule juu, umbali wa ghorofa zaidi ya hamsini yalifikaje na wakati hawakuwa na teknolojia yoyote ya kupandisha vitu vizito juu?

 

Leo ninakwenda kukuoneshea maajabu mengine ambayo inawezekana uliyajua au hukuyajua. Wengine wanasema za kishetani, wengine wanasema ilipangwa, kila mtu anasema lake, nani mkweli? Lilikuwa tukio la kupangwa au bahati mbaya, mpaka leo hakuna mtu anayejua.

 

Ni Septemba 11, 2001, majengo mawili ya WTC (Word Trade Center) yalilipuliwa jijini New York nchini Marekani. Kuna mengi kutokea kwa ishara mbalimbali. Kwa nini namba 11? Katika tukio hilo, namba 11 imetawala, namba hiyo katika ulimwengu wa giza inajulikana kama namba ya maono, yaani ni namba ambayo inatabiri kitu kitakachotokea hapo baadaye na ndiyo maana tukio hili limebeba sana namba hiyo kwa kuwa tangu kabla wao walijua lingetokea.

 

Tukio lilitokea Mwezi wa 9, tarehe 11. Wataalamu wa mambo wameanza na hii, ukiangalia hapo unaona namba tatu ambazo ukizichukua na kuanza kuzijumlisha utapata namba 11, yaani 9+1+1=11. Ukihesabu siku ya tukio, kwa mwaka 2001, Septemba 11 ni siku ya 254 ya mwaka, kwa hiyo ukichukua 2+5+4=11, unaipata ileile 11.

 

Wakati tukio hilo limetokea tarehe hiyo, zilikuwa zimebaki siku 111 mwaka kumalizika. Hapo utakuta 11 ipo kama kawaida katika siku hizo zilizobaki. Yalilipuka majengo mawili. Kila jengo lina ghorofa 110. Hapo 11 imetokea kwenye jengo. Lakini kulikuwa na jengo la tatu kuanguka. Hilo lilikuwa na ghorofa zake 47 ambapo 4+7=11. Maghorofa hayo mawili yalikuwa na madirisha 21,800, sasa chukua ujumlishe, yaani 2+1+8+0+0=11. Ndege ya kwanza kuligonga jengo la kwanza iliitwa Flight 11. Ndege hiyo ilikuwa na watu 92 ndani ambapo 9+2=11. Jengo la kwanza kushambuliwa, lilianza kuanguka saa 10:28, hapo ni 1+0+2+8=11. Majengo hayo yalijengwa kuanza mwaka 1966 mpaka 1977, kwa maana hiyo yalitumia miaka 11 kujengwa.

 

Majengo haya yapo sehemu inayoitwa Manhattan hapo New York. Sehemu hiyo iligunduliwa Septemba 11 na mtu anayeitwa Henry Hudson, ukichukua majina ya huyo jamaa, yana herufi 11. Hayo ndiyo maajabu ya namba 11 kwenye tukio la shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001, lililotokea jijini New York, Marekani.

 

NA: MWANDISHI WETU NA MITANDAO| UWAZI JUMANNE

Maajabu ya Dunia! Mti Ukikatwa Upande Unatoa Damu, Upande Unatoa Utomvu

Leave A Reply