Msanii wa Bongo Muvi Auzwa Kingono Nchini India

Msanii wa bongo Movie anayefahamika kwa jina la Suzan Michael ‘Prettykind’ akiwa nchini India.

 

MSANII wa bongo Movie anayefahamika kwa jina la Suzan Michael ‘Prettykind’ aliyewahi kucheza filamu mbalimbali zikiwemo Damu Yangu, Who is back, apple na Uyoga yamemkuta mazito baada ya kurubuniwa na kupelekwa kuuzwa nchini India, Risasi Jumamosi limezungumza naye na kufunguka.

 

Chanzo Cha habari hii Awali chanzo chetu ambacho kipo nchini India kiliwasiliana na gazeti hili na kudai kuwa, binti huyo mrembo ambaye kwa sasa yuko Bongo alifukuzwa huko baada ya kugonganisha wanaume wawili raia wa Nigeria na kusababisha balaa kubwa.

Suzan Michael ‘Prettykind’ akiwa njiani kurudi bongo akiwa nchini India.

Risasi lamsaka Kufuatia madai hayo, waandishi wetu walimsaka msanii huyo ambapo alipopatikana ndipo alipofunguka mazito yaliyomkuta maishani mwake ikiwa ni pamoja na kupelekwa kuuzwa India bila ridhaa yake. aeleza maisha yake kwa kifupi “Nakumbuka baada ya kumaliza darasa la saba Shule ya Msingi kule Magu, Mwanza nilijikuta kwenye maisha magumu sana, nikaamua kutoka Magu mpaka Mwanza Mjini kwa ajili ya kusaka maisha ambapo niliuza maji stendi na kufanya kazi za ndani.

 

“Baada ya kufanya kazi hizo za ndani ambapo manyanyaso yalikuwa mengi, nilipata kazi kwenye kituo cha televisheni cha Mwanza ambapo walikuwa wakirusha habari mbalimbali, nilifanya kazi pale kwa muda flani ambapo niliachishwa baada ya kufiwa na dada yangu. “Nilipoona mambo yamekuwa magumu, nilijiunga na Kikundi cha Filamu cha Tunda ambapo nilikuwa nikienda kufanya mazoezi ya sanaa, nikafanikiwa kwa kiasi flani kuigiza.

Akiwa kwenye pozi.

Alifkaje DaR? “Nikiwa kwenye harakati za kutafuta njia ya kuigiza, nilikutana na kaka mmoja ambaye aliniambia kuwa anamfahamu baba mmoja (jina linahifadhiwa) ana kampuni ya uigizaji atanisaidia. akutana na kigogo huyo wa filamu Msanii huyo anaeleza kuwa, alivyokutana na kigogo huyo wa filamu alijitolea kumsaidia lakini kwa sharti la kumpa penzi kwanza ambapo kwa tamaa yake ya kutaka msaada, alikubali ili pia aweze kuwa na ujanja wa kuishi mjini. “Nilitoa penzi bila kusaidiwa lolote mpaka nilipopata msukosuko wa kufukuzwa hotelini kwani kigogo huyo alikuwa hajalipa kodi ya hoteli kwa muda mrefu,” alisema. apangishiwa nyumba Akazidi kueleza kuwa, baada ya kuondoka hotelini, kigogo huyo wa filamu alimpangishia nyumba ikiwa ni baada ya kupelekewa askari na kulipa deni hotelini.

“Kiukweli alinifanya nikawa kama mke wake, nikasahau shida zote lakini siku moja nikiwa sina hili wala lile nilipigiwa simu na msichana mmoja ambaye alijitambulisha kuwa anataka kucheza filamu kwenye kampuni ya yule kigogo, bila kujua kuwa ni mkewe na alikuwa ananichota, nilimwambia asijali kwani mimi ni mtu wake. “Baada ya kumjibu vile yule mkewe, kigogo yule alikasirika sana, akanitelekeza na ndipo nilipoanza kuhangaika, nikawa nakwenda lokesheni kwa wasanii mbalimbali, nafanya kazi nalipwa vijisenti vya kujikimu.

 

Hatimaye nikarudi Mwanza baada ya maisha kuniwia magumu. abakwa na msanii “Nikiwa Mwanza alikuja msanii mkubwa ambaye kwa sasa ni mwanamuziki na alikuwa na filamu yake anaiandaa, akaniita ili nicheze kama mhusika mkuu, akaniambia niende hotelini alipokuwa kwa ajili ya mazoezi ili shooting ikianza nisisumbue. “Akawa ananifundisha, siku hiyo mara aniambie nivae taulo kuleta uhalisia lakini cha kushangaza alinisukumia kitandani na kunibaka, kitendo ambacho sitakisahau maishani.

ARUDI DAR TENA

“Baada ya kuhaha sana Mwanza, nilirudi tena Dar ambapo nilikutana na mwanaume mmoja aliyekuwa akifanya kazi Usalama wa Taifa baada ya kuniona gazetini ambapo nilitoa habari ya maisha yangu, akaamua kunisaidia ili nikutane na rais wakati huo alikuwa Jakaya Kikwete. “Mwanaume huyo alinishauri niandike barua ambayo niliiandika, nikaipeleka nikawa nasubiria majibu.”

Apigiwa simu ya Dili India “Nikiwa nasubiri majibu kutoka kwa rais, nilipigiwa simu na mtu ambaye namjua, akaniambia kuna kazi huko nchini India ambapo nitakuwa najiingizia pesa za haraka. “Kwa kuwa nilikuwa na shida ya pesa kwa ajili ya kutoa filamu, niliona kwanza nilifuate hilo dili kwani hata hivyo sikuamini kama rais angeweza kuniita. Nikasafiri mpaka India bila kujua ni kazi gani naenda kufanya. yamkuta makubwa Akizungumza huku akitokwa na machozi, Prettykind alisema kuwa, alipofika India alishangaa kuambiwa kuwa kazi aliyoitiwa ni kujiuza na kwamba angeweza kupata pesa nyingi kutokana na shepu yake. “Nilipoona nagombewa, kila mtu anataka kutoka na mimi, siku ya kwanza nilichukia sana, nikampigia simu yule mtu wa usalama wa taifa, nikamueleza kazi niliyoitiwa nchini India akanishauri niende ubalozini nikashtaki.

“Sikuwa nikijua wapi pa’ kukimbilia, sikuwa nikijua Kingereza wala sehemu yoyote zaidi ya nyumbani na kule nilikopelekwa kwa ajili ya kujiuza ambapo ni Club baada ya wanaume wengi kutumiwa picha zangu. “Kwa kweli nilijitahidi sana kufika Ubalozi wa Tanzania nchini India lakini kwa bahati mbaya siku niliyoenda sikupata msaada na ndipo nilipokutana na mama mmoja ambaye alinishauri niende nikatoe taarifa polisi.” afanya JitihaDa za kuRuDi bongo Baada ya kuona alichoitiwa India ni balaa, binti huyo alianza kupambana kurudi nyumbani lakini akakutana na vizingiti vingi ikiwa ni pamoja na yule aliyempeleka kumtaka amlipe shilingi milioni mbili, gharama alizotumia kumsafirishia hivyo akakwama. Akiwa inDia aitwa na Rais “Nikiwa India barua yangu ilijibiwa, nikaitwa na rais lakini sikuwa na njia kwani sikuwa na nauli.

Nikajaribu kumuomba yule aliyekuwa akinisaidia anilipie zile pesa lakini haikuwezekana, sikuwa na njia tena zaidi ya kubaki kule. afunDishwa kila aina ya ulevi Katika kushawishiwa aiweze kazi ile ambayo hakuizoea, aliambiwa anywe pombe avute madawa ya kulevya na sigara ndiyo ataiweza lakini vilevi vyote hivyo alivikataa na kuamua kujiuza kawaida kwani hakuwa na namna ya kufanya ili aweze kurudisha pesa za watu. “Nilijiuza kwa wanaume wanne kwa siku ili tu nifanikishe kupata pesa za kumlipa yule dada haraka. Nikiwa kwenye mishe hizo nilikutana na mwanafunzi wa Kinigeria, aliponinunua nikamweleza matatizo yangu, akanisaidia kunilipia, nikawa najiuza kwake yeye tu

mpaka nikamaliza deni, tukaamua kuishi wote,” anasimulia. mwanafunzi aonDoka, amuaChia Chumba “Yule Mnigeria alipoondoka aliniachia chumba ikiwa bado mwezi mmoja tu kodi iishe, ikabidi nirudie kazi ile ya kujiuza ili nipate pesa ya kujikimu kwani maisha ya kule bila kazi hayaendi. “Katika kujiuza nikapata bwana mwingine mtu mzima ambaye alinichukua nikakaa naye na kuachana kabisa na kazi ya kujiuza mpaka narudi Tanzania kwani alinisaidia sana.” apata gonJwa baya Msanii huyo anaeleza kuwa, katika kujiuza huko alipata gonjwa baya la kuwashwa na kutokwa na uchafu sehemu za siri hali iliyomfanya akose amani kabisa.

 

“Nilihangaika hospitali zote na kupatiwa matibabu nikapona ikiwa ni pamoja na kupima Ukimwi ambapo nilikutwa salama, namshukuru Mungu.” afiChua siRi nzito Prettykind alieleza kuwa, kuna baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao wamekuwa wakienda India kuuzwa kwa siri na wakirudi wanatesa mjini. “Siwezi tu kuwataja lakini wapo mastaa ambao nilikutana nao kule, nao wakijiuza tena wakati mwingine kwa bei chee, hali ngumu sana.” atoa somo kwa mabinti wenye tamaa Mlimbwende huyo alisema, lengo la kusimulia mkasa huu ni ili mabinti wenye tamaa ya kutafuta mafanikio kwa njia ya haraka wapate fundisho kwani kilichompata yeye asingependa kimpate mwingine. “Ni suala la kila mtu kujitambua na kutambua thamani yake, usikimbilie maisha mazuri kwa njia ambazo ni hatari. Na katika hili nitafungua taasisi yangu ya kuwashauri wasichana wanaopitia maisha magumu kama yangu, nitapita mashuleni na kila sehemu kutoa ushuhuda wa maisha yangu ili liwe fundisho kwa wengine. neno la mhaRiRi Prettykind amesikika, iwe funzo kwa wasichana wote wanaopenda maisha kwa pupa. Kwa anayeweza kumsaidia msanii huyu kufikisha ujumbe wake kwa wasichana wenzake nchini kote anaweza kuwasiliana na gazeti hili kwa namba zote zilizopo gazetini. Kumsikiliza Prettykind tembelea  globaltvtz.com” www. globaltvtz.com leo saa kumi na mbili jioni.

Stori: Hamida Hassan na Gladness mallya, DAR

Loading...

Toa comment