MREMBO mwenye shepu yake Bongo Movies, Amanda Posh amepangua uvumi uliozagaa mtaani kuwa, amezuiwa kuigiza na mchumba wake kwa kusema si kweli.
Amanda alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akipiga stori
na mwanahabari wetu ambaye alimbananisha swali kuhusu ukimya wake kwenye gemu na madai hayo ya kuzuiwa kuigiza.
“Bwana hawezi kunizuia kuigiza sema nilikuwa tu bize na masuala yangu binafsi ya kibiashara ndio maana kwa zaidi mwaka sasa nimekuwa kimya kwenye sanaa, ila nitarudi tu maana sanaa ndio kila kitu kwangu,” alisema Amanda.