The House of Favourite Newspapers

Q Chillah, Snura ‘live’ Tamasha la Full Dozi Dar Live

0
Snura Mushi ‘Mamaa Majanga.

KITANUKA! WAKALI wawili wasioshikika kunako gemu ya Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ na Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’ wanatarajiwa kuungana na wakali wengine kibao katika Tamasha la Full Dozi litakalofanyika Jumamosi hii (Septemba 9) ndani ya Uwanja wa Kimataifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema Full Dozi ni tamasha lililowaunganisha wasanii wa Muziki wa Dansi pamoja na Bongo Fleva huku akiwataka mashabiki na wadau wote wa burudani kujitokeza kwa wingi.

“Mbali na Q Chillah na Snura tutakuwa na mkongwe, Juma Nature, Beka Flavour, Sholo Mwamba, Dully Sykes wakati upande wa Muziki wa Dansi itakuwepo bendi kongwe ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Luiza Mbutu,” alisema Mbizo.

Kingilio katika tamasha hilo kitakuwa kiduchu yaani buku tano (5,000) tu getini.

Leave A Reply