The House of Favourite Newspapers

Jezi za Tshishimbi Zauzwa Kama Njugu Njombe

0
Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi.

JEZI za kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi tayari zimeanza kuuzwa kwa kiwango cha juu mkoani Njombe ikiwa ni siku chache kabla ya Yanga haijacheza na Njombe Mji kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani humo.

 

Njombe Mji na Yanga zinatarajiwa kupambana keshokutwa Jumapili ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Tshishimbi tayari ameshajizolea umaarufu kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha kwenye mechi yake ya kwanza hapa nchini dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii.

 

Jana Alhamisi, Championi Ijumaa lilizipata picha mbalimbali zikionyesha wafanyabiashara wa jezi katika Stendi Kuu ya Mabasi Njombe.

 

Licha ya kuwepo kwa jezi nyingi za wachezaji mbalimbali wa Yanga, lakini zenye jina la Tshishimbi raia wa DR Congo, ndizo zilikuwa nyingi huku ikisemekana kwamba ndizo zilizokuwa zikinunuliwa kwa wingi.  

Stori: Said Ally | Championi Ijumaa

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Kumbuka kuwa ili kujiunga na kubashiri ili kuvuna fedha unatakiwa kutembelea tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani una nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kuweka Sh 1,000 tu.

Leave A Reply