The House of Favourite Newspapers

Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi

0

LEO kwenye kona hii ya Mapishi tutaona jinsi ya kupika biriani ya nyama ya mbuzi.

MAHITAJI

Nyama ya mbuzi- kilo 1

Mchele- kilo 4

Vitunguu- 3 vikubwa

Nyanya- 2

Nyanya ya kopo- vijiko 3 vya chakula

Kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa -vijiko 2 vya chakula.

Biriani masala (mchanganyiko wa bizari kwa ajili ya biriani )- vijiko 2 vya chakula.

Hiliki- kijiko 1 cha chai

Chumvi- kiasi

Mafuta- ½ kikombe

Zaafarani au rangi za biriani tofautitofauti.

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA SOSI YA NYAMA KWANZA

Changanya nyama na kitunguu swaumu, chumvi na biriani masala. Weka kwenye moto hadi viive.

Baada ya hapo, weka mafuta katika kisufuria kingine kisha andaa vitunguu hadi vigeuke rangi. Baada ya hapo, tia nyanya ya kawaida, nyanya ya kopo na bizari zote nyingine zilizobakia. Ukimaliza, changanya na ile nyama yako uliyokuwa unachemsha au kuoka kwa wale wenye jiko la oven, kwa kufanya hivyo, utakuwa umepata mchuzi wako mzito wa biriani.

JINSI YA KUPIKA

Chukua mchele wako wa basmati, mdalasini kijiti kimoja, hiliki tatu kisha tia na chumvi, baada ya hapo, weka kwenye moto. Funika upike hadi nusu kiini kisha uchuje kwa kumwaga maji.

Tia mafuta kidogo katika mchele na zaafarani iliyolowekwa au rangi za biriani kisha rudisha mchele katika sufuria ufunike na upike hadi uive.

Pakua wali katika sahani kisha mwagia sosi ya nyama juu yake, pambia kwa kukatia nyanya na pilipili. Kwa hatua hizo chakula chetu kipo tayari kwa kuliwa.

Leave A Reply