The House of Favourite Newspapers

Farhia Middle Hoi Kwa Aslay!

0
Mtangazaji ‘bei mbaya’ wa Vituo vya ITV/ Radio One, Farhia Hussein Middle.

MTANGAZAJI ‘bei mbaya’ wa Vituo vya ITV/ Radio One, Farhia Hussein Middle amesema kuwa, miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva anaowazimikia ni pamoja na Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ kutokana na umahiri wake wa kutunga na kuimba nyimbo zenye kugusa hisia na kumtabiria kuwa atafika mbali kwenye safari yake ya kimuziki.

Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’.

Akibadi-lishana mawazo na Showbiz Extra juu ya burudani za muziki na filamu Bongo mwanzoni mwa wiki hii, Farhia ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kusoma taarifa ya habari kupitia ITV/Radio One alisema kuwa, tangu aanze kufuatilia muziki huo hajawahi kuguswa na tungo za mashairi kama ilivyo kwa Aslay huku akitumia nafasi hiyo kumshauri asibweteke, badala yake aongeze juhudi na ubunifu wa nyimbo zinazoelimisha jamii.

“Ngoja niwe mkweli, kwa wasanii wa Bongo Fleva, anayenigusa sana ni Dogo Aslay, ninampenda sana huyo kijana kutokana na ufundi wake kwenye muziki maana anaachia nyimbo nyingi nzuri kwa wakati mmoja, ninampenda mdogo wangu na ninamshauri aongeze juhudi aweze kupiga hatua zaidi, lakini bahati mbaya wasanii wetu wakipata mafanikio kidogo tu, wanaridhika, japo ninamuona Aslay yuko tofauti na Mungu atamsaidia,” alisema Farhia ambaye pia anaongoza Kipindi cha Mazungumzo ya Familia cha kila Jumapili kupitia Radio One.

 SOMA:Pendo Aibuka, Ataja Sababu Za Kuchukia Mapenzi!

Leave A Reply