The House of Favourite Newspapers

Polisi Dar: Hatukukamata Waliovaa Fulana za Tundu Lissu

0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa.
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema watu waliokamatwa na polisi hapo jana kwa kufanya mkusanyiko usio rasmi, walishaonywa kutofanya hivyo lakini hawakujali hivyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yao.
Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi.
Kamanda Mambosasa amesema hayo leo  na kusema  kitendo cha kufanya mkusanyiko usio rasmi ni kuvunja sheria, hivyo lazima watafikishwa Mahakamani kujibu shtaka lao, huku akikanusha kuwakamata watu hao kwa kutokana na kuvaa t-shirt zilizoandikwa ‘pray for Tundu Lissu’.
Polisi wakiwa doria.
“Kwanza ifahamike hatujawakamata kwa kosa la kuvaa tshirt, zile ni nguo kama nguo nyingine wanavyovaa mashabiki wa Simba na Yanga, hawa walichofanya mpaka wakamatwe ni kufanya mkusanyiko usio rasmi na kibaya zaidi tulishawaeleza, na wenyewe walipoona polisi wanakuja wakaanza kutukimbia kwamba walijua wamefanya nini”, amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kusema jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao na kisha kupelekwa Mahakamani kusomewa mashtaka yao ili sheria ifanye kazi yake.

KIMENUKA! Polisi Walivyowatimua Chadema Kwenye Ibada Ya Lissu

Leave A Reply