The House of Favourite Newspapers

Maumivu ya Mgongo tatizo linalosumbua Wengi – 03

0

MATIBABU NA USHAURI

 

Matibabu ya mgongo mara nyingi ni kwa njia ya upasuaji pia yanaweza kufanyika pale chanzo cha tatizo kinapobainika kuwa ni uvimbe au mteguko unaogandamiza mishipa ya fahamu.

 

Njia nyingine ni vidonge na kufanyishwa mazoezi maalumu kulingana na mtaalamu atakavyopendekeza kulingana na eneo la uti wa mgongo, lililoathirika.

 

Endelea nayo NI muhimu kula mlo kamili wenye viinilishe muhimu vinavyoimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Ni vizuri kujiepusha na utumiaji wa chumvi nyingi kwenye chakula, matumizi ya pombe kupita kiasi ili kukwepa tatizo la kudhoofika kwa mifupa.

 

Ni vema pia kuachana na uvutaji wa sigara na matumizi mengine ya tumbaku kwani sumu zilizomo husababisha mishipa midogo inayopeleka damu mgongoni isinyae na kusababisha upungufu wa hewa ya oksijeni na viinilishe muhimu kwa ajili ya afya ya viungo hivyo. Kufanya mazoezi ya mwili kama vile kutembea, kuogelea, kujinyoosha, kupiga pushapu na kukimbia ni muhimu ili kupunguza unene na maumivu ya misuli ya mgongo.

 

USHAURI KWA WAJAWAZITO

 

Wajawazito wanashauriwa kufanya mazoezi mepesi ya aina ya ‘Pelvic Rocking’ ambayo yanahusisha kuinama kwa kupiga magoti na kuweka viganja vya mikono chini huku akiinua mgongo juu taratibu. Wanawake wanaovaa viatu vyenye visigino virefu wakiwa na ujauzito wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa kuacha kuvivaa hasa pale wanapolazimika kutembea muda mrefu. Njia nyingine inayosaidia ni kukaa na kulala kwa namna inayofaa.

Ni vizuri pia kuepuka ubebaji wa vitu vizito kupita kiasi ili kuepuka matatizo yanayoweza kuumiza uti wa mgongo kwa namna moja au nyingine.

Na Dk. Marise Richard

MWISHO

Leave A Reply