The House of Favourite Newspapers

Sabby: Hamisa Pigania Ndoa Sasa

0
Sabrina Omary ‘Sabby Angel’

MSANII wa filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amemtaka mwanamitindo Bongo, Hamisa Mobetto kupigania ndoa kwa Mbongo Fleva aliyezaa naye, sababu dini yake inamruhusu kuwa mke wa pili.

Hamisa Mobetto

Akipiga stori na Star Mix, Sabby alisema kuwa, pamoja na yote yaliyotokea ni vyema mwanadada huyo asivunjike moyo kama bado anamuhitaji mzazi mwenziye huyo, licha ya kuonekana ameelemea kumuhitaji Zarinah Hassan `Zari Boss Lady’ anapaswa kukomaa hadi ndoa ifungwe.

 

“Namshauri Hamisa asikubali kirahisi kumkosa baba wa mtoto wake, kama vipi huyo jamaa awaoe wote wawili Zari mke mkubwa na Hamisa mke mdogo maana dini imeridhia wake hadi wanne,”alisema Sabby.

Leave A Reply