The House of Favourite Newspapers

Pspf Yawazawadia Wafanyakazi Wake Kwenye Kilele Cha Wiki Ya Huduma Kwa Wateja Duniani

0
Bw. Mayingu akimpatia zawadi Afisa Mipango Miji wa kampuni mshirika na PSPF, Ardhi Plan Limited, Bi. Anna Lukindo.
Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto)
Mkurugenzi Mkuu na viongozi wengine wa Mfuko wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa tuzo
Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Bi.Valley Malinga
Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Elizabeth Shayo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi “waliochomoza” kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia wateja, (wanachama) wa Mfuko.
Bw. Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017.
 
 
Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja.
“Wakati nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu.” Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. 
 
 
Bw. Mayingu aliwapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo kote nchini, kwa kazi nzuri na kuwaeleza kuwa kitendo cha wafanyakazi na maafisa wa Mfuko huo kutoka maofisini na kuwafata wateja, (wanachama) majumbani kwao ili kuzungumza nao na kuwahudumia kimesifiwa sana.
 
“Kaimu Mkurugenzi Mkuu, alifuatana na baadhi yenu kwenda kule Kipunguni B. na kukutana na mwanachama wetu, Bw. Kassim Mafanya, ambaye alikipongeza kitedo kile na kusema hakutegemea maishani mwake yeye kama mstaafu angetembelewa nyumbani kwake na PSPF, hili ni jambo jema.” Alibainisha Bw. Mayingu.
Wafanyakazi waliopata tuzo ni Elizabeth Shayo, kutoka kitengo cha Huduma Kwa Wateja, Makao Makuu, ambaye kupitia teknolojia, (mifumo), ni wateja wenyewe ndio waliompendekeza kutokana na maoni yaliyopokelewa lakini idadi ya watu aliowahudumia.
 
Mwingine ni Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), ambaye naye alitunukiwa tuzo na kupewa zawadi kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wateja bila kuchoka.
Tuzo hizo pia zimekwenda kwa walezi wa mikoa wa PSPF, kampuni mshirika ya Ardhi Plan Limited na pia makampuni washirika yaliyoshirikiana na PSPF kwenye wiki ya huduma kwa wateja, ambayo ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mabenki ya CRDB, NMB, TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB).
Leave A Reply