The House of Favourite Newspapers

Wakubwa Wala Vichapo NBA

0

UZI Jumapili ilikuwa ni siku ya kusha-ngaza na kufura-hisha katika michezo ya Ligi Kuu ya Kikapu Marekani (NBA), hasa baada ya timu nyingi kubwa kupokea vipigo kutoka kwa timu ndogo ambazo wengi waliingia viwanjani wakijua zinakwenda kufungwa.

 

Pistons yaichapa Warriors

Detroit Pistons ilisafiri kwenda Oakland, California na ikafanya kazi vizuri kwa kuwachapa mabingwa watetezi, Golden State Warriors kwa pointi 115-107. Avery Bradley alifunga pointi 23, Reggie Jackson akafunga 22 na kutoa asisti tano, na Andre Drummond alimaliza akiwa na mipira iliyorudi, kwa maana ya rebounds 18, pointi nane na asisti tano.

 

Klay Thompson aliiongoza Golden State kwa kufunga pointi 29, Kevin Durant akafunga pointi 28, rebounds sita na asisti nne, Stephen Curry 27, rebounds sita na asisti nane, wakati Draymond Green aliongeza rebounds 13 na asisti nne.

 

Knicks yaiua Cleveland

New York Knicks yenyewe iliichapa Cavaliers kwa pointi 114-95 jijini Cleveland. Tim Hardaway Jr alifunga pointi 34, rebounds nne na asisti nane, Kristaps Porzingis pointi 32, rebounds 12 tena dabodabo, Enes Kanter pointi 18, rebo-unds 12 dabo-dabo, na Courtney Lee pia alikuwa na dabodabo kwa pointi 15 na rebounds 10.

Cleveland Cavaliers, maarufu kama Cavs, wenyewe waliongozwa na Kevin Love aliyefunga pointi 22, rebounds 11 dabodabo, LeBron James alifunga pointi 16, rebounds 12 dabodabo, Derrick Rose pointi 15, na Kyle Korver alimaliza akiwa na pointi 13 na rebounds nne.

 

Hornets nayo yaigonga Magic

Charlotte Hornets iliichapa Orlando Magic kwa pointi 120-113 kwa msaada mkubwa wa pointi 34 za Kemba Walker, aliyepiga pia asisti 10. Dwight Howard alikuwa na pointi 22 na rebounds 10, Jeremy Lamb pointi 20, rebounds sita na asisti saba, wakati Marvin Williams alimaliza akiwa na pointi 13 na rebounds 11.

Jonathan Simmons aliiongoza Orlando kwa pointi 27 na rebounds nne, fowadi Mfaransa mwenye asili ya Algeria, Evan Fournier alikuwa na pointi 23 na asisti tano, Aaron Gordon 17, rebounds tisa na asisti nne, na Nikola Vucevic pointi 15, rebounds 11 dabodabo.

 

Pacers yaichapa Spurs

Mlinzi Mmarekani mwenye asili ya Nigeria, Victor Oladipo alifunga pointi 23, rebounds nne na asisti tano, na kuisaidia Indiana Pacers kuifunga San Antonio Spurs kwa pointi 97-94. Domantas Sabonis alikuwa na pointi 22, rebounds 12 dabodabo, Bojan Bogdanovic 15 na rebounds nane, wakati Thaddeus Young alimaliza akiwa na pointi 12 na rebounds tano.

 

San Antonio iliongozwa na LaMarcus Aldridge aliyefunga pointi 26 na rebounds nane, Pau Gasol alikuwa na pointi 17, rebounds saba na asisti tano, wakati Danny Green, Patty Mills na Rudy Gay kwa pamoja walifunga pointi 30 huku kila mmoja akitupia pointi 10.

 

Kwingineko

Fowadi Mgiriki mwenye asili ya Nigeria, Giannis Antetokounmpo alifunga pointi 33, rebounds 11 dabodabo katika ushindi wa 117-106 ambao Milwaukee Bucks waliupata dhidi ya Atlanta Hawks, Washington Wizards wenyewe waliifunga Sacramento Kings kwa pointi 110- 83, huku Denver Nuggets wakiichapa Brooklyn Nets pointi 124-111 kwa mkono wa Nikola Jokic aliyefunga pointi 21 na rebounds 14 dabodabo.

Leave A Reply