The House of Favourite Newspapers

Mastaa Kiboko Kwa Kubadili Nywele Za Gharama Bongo

0
Kajala Masanja

MASTAA wengi Bongo,kitu kikubwa wanachopenda ni kuonekana bomba kwenye vichwa vyao ambapo mara nyingi utawaona wamebadilisha mitindo mbalimbali ya nywele.

 

Kumekuwa na aina nyingi za nywele lakini mastaa wana sehemu zao maalumu na wanajua wapi wanaweza kupata nywele zenye ubora ambazo kila wanapoweka kichwani wanasifiwa na kutoka bomba.

Wema Sepetu

Kati ya mastaa ambao wanaongoza kwa kuweka nywele za gharama kwenye vichwa vyao huku wakiwa hawana desturi ya kuzirudia kichwani ni Kajala Masanja, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Shamsa Ford, Shilole na Odama.

Jacqueline Wolper

Mastaa hawa mara nyingi wanashonea na kuvaa mawigi aina Peruvian na Human ambayo ndiyo yenye ubora mkubwa na mara nyingi bei zake huwa juu kuanzia laki tatu mpaka milioni moja.

Elizabeth Michael ‘Lulu’

Ukiangalia kwa mmoja mmoja, matumizi wanayotumia katika nywele zao kwa mwaka mzima yanaweza kufika hata milioni kumi na zaidi kwa sababu wengi wao hawarudii na wakati mwingine wanataka za tofautitofauti kuendana na fasheni. Ukimchukulia mfano mzuri, Wema Sepetu hata katika picha zake mbalimbali, huwezi kumkuta karudia nywele na mara nyingi anazoziweka kichwani ni kuanzia laki tano na zaidi huku akifuatiwa na Kajala. Binafsi nilishawahi kumshuhudia Kajala akinunua nywele ya milioni moja na nusu maeneo ya Namanga jijini Dar, ndani ya miezi miwili hakuwa nazo.

STORI: IMELDA MTEMA, IJUMAA

Leave A Reply