The House of Favourite Newspapers

Lwandamina Hacheki, Hanuni Lakini…

0
Kocha wa Yanga, George Lwandamina.

KILA mmoja anaweza kuwa na aina yake ya kila kitu, hii inatokana na namna Mwenyezi Mungu alivyotuumba ingawa kuna mambo mengine yanaweza kuwa ni maamuzi ya mtu binafsi.

 

Kwamba mmoja ana tabia za maneno mengi, mwingine ni mkimya na mwingine ana aina nyingine. Kunaweza kukawa na mambo ya kisayansi lakini bado msukumo wa uamuzi wa mtu binafsi unaweza ukawa ni muundo unaotoa taswira ya mtu fulani.

Uchunguzi wangu mdogo unanionyesha wapenda soka wengi wa Tanzania, wangependa sana mchezaji mwenye kasi na makeke hata kama angekuwa hafungi mabao badala ya yule anayekimbia kwa spidi ndogo hata kama anafunga mabao zaidi.

 

Yule anayekimbia na kusim-ama, akaon-doka akitingi- shika kwa mbwembwe nyingi, anaweza kuwa kivutio zaidi kuliko yule anayeweza kwenda kukaa katika nafasi akisubiri krosi halafu akafunga kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yake.

 

Watanzania wanapenda watu machachari na kitu kibaya zaidi, wengi huamini mtu machachari ndiye mtendaji bora zaidi. Inawezekana asiye na machachari akawa na utendaji bora zaidi maradufu.

 

Mimi ningependa tujifunze kupitia Kocha wa Yanga, George Lwandamina. Huenda akawa hawafurahishi watu wengi kutokana na mwonekano au mwenendo wa utendaji wake wa kazi.

 

Anaonekana ni kama mtu mtaratibu, unaweza kumuona ni kama mzembe sana na kwa kuwa unavutiwa na watu machachari, hauwezi kufurahishwa na mwenendo wake wa mambo anayofanya.

Lwandamina ni mtaratibu sana na inawezekana ni mara chache unaweza kumuona akiwa anafoka. Muda mwingi ataonekana akiwa amekaa tu kama mtu aliyechoshwa na jambo na anajaribu kutafakari itakuwaje.

Majibu ya kile anachokifanya kinapatikana katika majibu sahihi mwisho wa jambo. Utaona tayari ana rekodi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara hata kama alimalizia kazi ya Kocha Hans van Der Pluijm ambaye leo anakutana naye kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Bara, Mholanzi huyo akiwa na kikosi cha Singida United.

 

Utakumbuka, Lwandamina hakuwa chaguo la Wanayanga wengi ambao walikuwa wamemzoea Pluijm na walitaka lazima aondoke kwa kuwa waliona kama anawakwamisha na wengine waliamini timu haichezi kwa kushambulia sana kama walivyotaka. Mwisho yeye pamoja na ugeni wake akabeba ubingwa na kumaliza kelele zote.

 

Pia kumbuka wakati anabeba ubingwa, kikosi cha Yanga kilikuwa katika msukosuko mkubwa ikiwemo mwishoni kujiuzulu kwa mwenyekiti wake, Yusuf Manji ambaye pia alikuwa ndiye mfadhili mkuu. Aliendelea kusaidia kiaina lakini haikuwa kama ilivyokuwa akiwa mwenyekiti, mambo yalikuwa na uhakika hasa kipindi cha Pluijm.

 

Msimu huu umeanza, kikosi cha Simba kikaonekana ni tishio zaidi na Yanga haikuwa na nafasi tena. Haikuwa na usajili wa kutisha zaidi ya kuongeza baadhi ya sehemu ambazo zilionekana zinatakiwa kuongezewa watu.

Hakuwa na usajili wa mbwembwe na wala hakuwa na makuu sana. Hadi leo, Yanga iko katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi nane sawa na vinara wa ligi hiyo Simba ambao pia wana pointi 16.

 

Ukiangalia mechi ya mwisho, pamoja na Simba kuonekana ni timu hatari, mwisho wa mchezo, Yanga ilionekana ilishambulia zaidi na mashambulizi makali zaidi ya kushitukiza.

 

Yanga ndiyo ilionekana kujilinda zaidi ya Simba, ikashambulia zaidi ya Simba na mwisho wa mechi ikawaachia presha kubwa Simba ambayo inaendelea kuunguruma hadi leo na huenda wataipoza kesho baada ya mechi yao mjini Mbeya.

 

Angalia sasa Lwandamina anatumia vijana ambao huenda hata hawakuaminika kama Raphael Daud, Pius Buswita, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya na wanaendelea kuifanya Yanga ionekane ni bingwa mtetezi anayepambana kuhakikisha analitetea taji lake maana hadi mechi ya nane, yuko katika njia sahihi. Akiteleza, bado inaon ekana ana weza kuamka na Wana yanga wanaweza kuwa na pande mbili, za kumkwamisha au kumsaidia kufanya vizuri zaidi kwa kuwa inaonekana kazi yake anaijua kweli.

 

Sisemi nina uhakika na Lwandamina atafanya vizuri sana au atachukua ubingwa, lakini najifunza namna mtu anavyoweza kufanya kazi zake kwa utulivu na akafanikiwa.

 

Lwandamina kwangu ni mfano mzuri wa pili kutoka Zambia kwa mfumo alionao. Kocha wa kwanza kuwa mfano alikuwa ni Patrick Phiri aliyewahi kuifundisha Simba kwa nyakati tofauti.

Kwamba bado tunatakiwa kujifunza kwamba papara na makeke machoni mwa watu si lazima uwe ndiyo utendaji bora. Badala yake majibu yanayotokana na kazi ndiyo kinapaswa kuwa kipimo sahihi cha mtendaji.

MAKALA: SALEH ALLY | CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave A Reply