The House of Favourite Newspapers

Ester Kiama Aomba Baraka Kwa Watoto Yatima

0
Staa wa Bongo, Ester Kiama.

MUIGIZAJI anayekuja vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Ester Kiama, juzi alikwenda kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa katika Kituo cha Watoto Yatima cha Ijango Zaidia, kilichopo Sinza Madukani, ikiwa ni pamoja na kuomba baraka k u t o k a kwao ili m a m b o yake yaweze kufanikiwa.

Akizungumza na Kilinge, Ester alisema hakuwa na kikubwa lakini amejifunza kuwa wakati anaenda kusherehekea ukumbini na watu wengine ambao wanajiweza kwa kila kitu, basi ni vizuri kabisa kuwakumbuka na watoto ambao wana uhitaji wa mavazi, chakula na vitu vingine muhimu.

“Kufanya hivi nimefarijika sana kwa sababu haina maana kwenda kufurahia ukumbini kula na kunywa huku kuna watoto wadogo ambao hawana wazazi wala msaada wowote wapo tu na ninaamini kwa hiki kidogo nimepokea baraka nyingi kutoka kwao,” alisema.

STORI: IMELDA MTEMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply