The House of Favourite Newspapers

Mobeto Aumbuka Mahakamani, Timu Zari Full Vicheko

0
Video Queen matata Bongo, Hamisa Mobeto.

 

VIDEO Queen matata Bongo, Hamisa Mobeto ameumbuka baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa na mzazi mwezake juu ya matunzo ya mtoto Abdul Nasibu ‘Prince Dully’.

 

Uamuzi huo umetolewa jana (Ijumaa) na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.

Mfanyabiashara maarufu Zarina Hassan maarufu Zari Thebosslady

Awali, Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys ambapo pamoja na mambo mengine aliomba matunzo ya mtoto aliyempata kwa kushirikiana na msanii huyo.

 

Mobeto akaiomba mahakama imwamuru mzazi mwezake huyo kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi ya shilingi milioni 5 sambamba na kumuomba msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

 

Kufuatia kesi hiyo, mwanaume aliyezaa na Mobeto ambaye ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.

Aidha, msanii huyo aliwasilisha hati ya majibu akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai kiasi cha pesa anachodai kulipwa kwa mwezi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa na hawezi kumudu.

 

Wakati huohuo, juzikati mtoto wa Hamisa Mobeto, Prince Dully alitimiza umri wa miezi mitatu tangu alipozaliwa na kama kawaida, mama yake akatupia picha zake katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram na kumpongeza.

 

Baada ya kutupia picha hizo, mashabiki zake wakaipokea na kuipiga zengwe, wakitoa madai kuwa sura ya mtoto huyo haifanani na baba yake huku

wakiweka picha ya mtoto huyo na baba yake wakionyesha kutofanana.

‘Mashabiki hao maandazi’ walienda mbele zaidi kwa kumtaka mzazi mwenziye na Mobeto kuchukua vipimo vya vinasaba maarufu kama DNA, kwani huenda amepigwa changa la macho.

 

Risasi Jumamosi liliamua kuchimba habari hizo kwa kirefu kwa kutumia vyanzo vyake mbalimbali na kubahatika kukutana na mmoja aliyekuwa na ubuyu ulioenda shule.

 

“Nyie mnaona leo, mbona mama mkwe wake Mobeto alishaliona hilo jambo kitambo tu, alikwenda kumtazama mtoto, alipomuona akaona kabisa pale damu ya mwanaye haipo.

 

“Kama unafuatilia posti za mama mkwe, utagundua kuwa baada ya kuona hilo changa la macho, akajiweka kando, akaanza kutupia picha za wajukuu zake wa Sauzi na kurusha vijembe,” alidai.

 

Baada ya mama mkwe kutopatikana hewani, Risasi Jumamosi liliwasiliana na baba mkwe wa Mobeto, Abdul Jumaa ili kusikia maoni yake juu ya tuhuma zinazotolewa na ushauri kwamba mtoto huyo wa pili wa mwanamitindo kuzaa na wanaume tofauti, akapimwe DNA ambapo alisema:

 

“Mimi ninachojua wote ni wajukuu zangu, mbona mtoto wa Zari alisemwa sana apimwe DNA lakini hakupimwa na mwisho ukweli umeonekana? Mimi ninachosema ninawatambua wote kama wajukuu zangu, sitaki kabisa kuongelea tena mambo hayo DNA…. DNA… kila siku, naomba watu wawaache wajukuu zangu.”

 

Baada ya kuzungumza na baba mkwe, Risasi Jumamosi lilimwendea hewani Mobeto na kutaka kusikia maneno yake juu ya ishu hiyo ya DNA ambapo kwanza alicheka kisha akasema:

“Jamani nimechoka na hizi habari, niacheni nipumzike, nitakutafuta baadaye nikujibu maswali yako.”

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Mobeto, mashabiki wa Zari wanaofahamika kama Team Zari, wanaangua kicheko huku wakiweka picha mbalimbali za mtoto huyo na kusindikiza na ujumbe wa shombo, wakishadadia suala la kupimwa DNA.

 

Pia wakaupokea ‘kishambenga’ uamuzi wa Mahakama ya Kisutu wa kutupilia mbali madai yake dhidi ya mzazi mwezake.

Leave A Reply